Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,782
- 239,461
Iko wazi sasa kwamba nchi hii haina uwezo wala mikakati yoyote ya kuboresha timu yake ya Taifa , wala hakuna kiongozi yeyote ( wa soka wala wa kisiasa ) mwenye uchungu na anayeweza kuona aibu kwa vipigo vya fedheha ambavyo timu yetu inawaletea wananchi na mashabiki wa soka kwa ujumla .
Kocha kama mkwasa aliyeleta aibu ya kutandikwa bao 7 na Algeria hawezi kuleta mabadiliko yoyote kwenye soka katika nchi yetu , siku zote kocha anayefanya vibaya hutimuliwa mara moja , no excuse !
Sasa ukiona nchi ambayo kocha anabaronga halafu analindwa , eti kwa vile ni mzalendo , basi ujue kabisa nchi hiyo haifahamu kwanini imeingia kwenye mashindano , Hivi ni uzalendo gani wa kuleta aibu na majonzi katika Taifa ?
Ushauri wangu kwa nchi hii kama mzalendo mwenye uchungu na nchi yangu , timu hii iondolewe kwenye michuano yote ya kimataifa kwa kipindi cha miaka mitano ili tujipange upya na kutafakari Mustakabali wetu.
Nakala kwa Jamal Malinzi na Nape Nnauye .