Ushauri tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri tafadhali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Prince Nadheem, Sep 10, 2012.

 1. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Habari za leo ndugu zangu?? jamani nina rafiki yangu mmoja wa kike ( just a friend and nothing else ) ambae amekuwa na wakati mgumu katika kila uhusiano wa mapenzi aliowahi kuingia. Alikuwa na BF wa kwanza miaka 4 iliyopita dada akampenda sana na ilonesha kama vile wanapendana lakini mwisho wa siku mambo hayakuwa kama ambavyo wengi tulitegemea. Jamaa alipata scholarship ya kwenda kusoma India,alipofika tu akamwambia dada kuwa hawezi kuendelea kuwa nae katika aina hiyo ya mahusiano ( plutonic/distant love ) so ikawa ndio game over kwa mtindo huo. Kutokana na kitendo kile akajikuta kuwa anaingia kwenye uhusiano na mtu mmoja ambae hapo awali aliwahi kumtokea ila alianika kuwa japo anamtokea ila just for fun kwani nae ana GF wake ambae wanapendana sana,ila as the time went on huyu rafiki yangu akaanza kufall seriously in love with that guy ambae iliokuwa ni just for fun ila jamaa alipoanza kumchoka akaanza kum-mistreat to the extent dada akashindwa kabisaaaaaa...... kutokana na hali hiyo ya mikasa huyu rafiki yangu alichanganyikiwa sana but I did my level best as her best friend kumshauri na kuwa nae karibu kwa namna ambayo mi niliona kuwa inafaa. So alikaa nje ya mahusiano kwa takribani miaka 2 huku akiuguza majeraha yake ya mapenzi. Mwaka huu mwezi wa 4 alikuja siku hiyo na kunambia kuwa kuna jamaa alikuwa anamfukuzia kwa takribani miezi sita so she thinks the guy was so much committed na labda anaweza kuwa ndie Mr nice guy wake,nilimwambia angoje na kumchunguza before taking him to the next level. Mwezi wa sita akanambia ya kuwa wana appointment hotel ya white mark in order to get to know each other better. I wished her the best of luck and she went. kwa kweli mwanzo rafiki yangu huyu alichanganyikiwa akisema hajawahi kuwa na mwanume ambae yupo so much in love with her like this one. mwezi wa saba huyu rafiki yangu alipata likizo ya mwezi kazini kwake so akaenda mwanza lakini jamaa alikuwa mkali kuwa hawezikaa pekee yake kwa muda mwezi,dada alikaa mwanza siku 3 tu akarudi Dar siku ya 4 na mapenzi yao yaliendelea kama kawaida. mwezi uliopita sasa jamaa akaanza kupunguza mawasiliano,dada akiuliza jamaa anajibu kuwa yupo bize na shule ( anafanya CPA ). Jambo la kushangaza ni kuwa awali jamaa wakati ndio anafukuzia mzigo alikuwa hata kama ni saa mbili za usiku ni lazima amsindikize dada kwake Chanika all the way from Mwenge siku yeyote ya juma au hata kwenda kumfuata for outing na hapo jua kuwa jamaa hana gari so nae ni mzee wa public transport (daladala). So by then alikuwa hayo yote anayaweza!!!!! tukirudi katika hali ya sasa dada baada ya kuona ya kuwa it is getting so serious nae akaamua apunguze mwasilino aone kama jamaa atashtuka. It was a deadly mistake!! mwasiliano ndio yakafa kabisa ila baadaye jamaa akampigia dada simu kuwa kwanini hali inakuwa vile so yabidi watafute muda waende kuongea. dada akajipanga kwa hayo maongezi na jamaa akapendekeza kuwa dada aende kwake wakaongee yaishe. Siku ilipofika sasa dada kaenda hadi Mwenge kwa jamaa si ndio kukuta jamaa hayupo ingawa dada anafunguo yake ya ndani kwa jamaa so aliingia hadi ndani. Kumpigia simu jamaa akajibu kwa kauli fupi tu kuwa alipata dharura na jamaa akakata simu japo yeye ndio kapigiwa. Dada alikaa tangu hiyo saa tano aliyoenda hadi saa tisa alasiri,hakuna mtu wala simu kutoka kwa jamaa! basi dada akarudi zake nyumbani kwa unyonge huku analia,maana alinipigia simu huku analia kuwa jamaa kabadilika kuliko kawaida. basi jamaa siku ya pili ndio anapiga tena simu akiomba waonane tena kwake,dada akamwambia "nilikuja kwako hutakaniona ukaondoka so kama kweli sasa unayo nia ya kuonana na mimi njoo Chanika this weekend. Jamaa alikubali likini cha kusikitisha sasa jana ilikua ni weekend ya pili na jamaa hajaonekana na mawasiliano ndio kama hivyo hadi ajiskie na sababu kubwa jamaa anadai kuwa yuko busy. Dada analia na leo navyopost huu uzi dada hajaenda kazini yupo home anaumwa ila mi najua ni stress na anashindwa kuelewa either aendelee na jamaa au?? mi ningemshauri kuwa aachane nae ila naona kama this is way too early for that advice. naomba mchango wenu ili nipate complete set ya ushauri wa kwenda kumpatia rafiki yangu huyu maana kaniomba nikitoka job nimpitie kwa ushauri zaidi. AHSANTENI SANA na samahani kwa uzi mrefu but that was for making sure that there is no missing part in it.
   
 2. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yani kwanza nampa congrats za kupenda wanaume wanne kwa speed kali kama hio.

  Si unajua namna anavyo kwenda speed ndo anavyo kuwa hatarini.

  Asije wamaliza wanaume wote tu kwa speed anazo kwenda:bounce:
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  ninachoweza kusema ni kifupi tu...mwambie huyo dada aache kupenda upendo wa MKE KWA MUME, bali apende UPENDO WA MATARAJIO. Hili kosa wanawake wengi wamekuwa wakifanya na wamekuwa wakitendwa
   
 4. GIUSEPPE

  GIUSEPPE JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 4,473
  Likes Received: 4,482
  Trophy Points: 280
  gush, nimesoma yote lakini kwa shida sana, jifunze kupangilia maandiko yako, sisi watu tunao vaa vioo usoni shida tupu
   
 5. MASELE

  MASELE JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  asa wewe mtoto wa mfalme, si umsaidie wewe aka muoe
   
 6. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Asimfuatilie tena huyu mwanaume, mwambie ajipe muda wa break kutoka kwenye mahusiano, aangalie nyuma where she went wrong.........mapenzi yatakuja kwa muda sahihi, japo anaumia lakini ni vyema akamwacha huyo mwanaume
   
 7. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  natoa pole sana kwa dada, MAHUSIANO Yanahitaji uvumilivu ni ukweli usiopingika jamaa kampotezea...endelea kumfariji
   
 8. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hebu weka paragraph pliz
   
 9. miss wa kinyaru

  miss wa kinyaru JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 543
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyo mwanaume wala hana mapenzi tena, aachane nae, tena mwambie afute no yake ya simu kabisa ili aachane na mawasiliano, akipigiwa amuulize nani mwezangu, akimuuliza mara mbili hatapiga tena, na yeye itamsaidia kusahau taratibu,kwasababu anapopigiwa ndio kidonda kinatoneshwa na kujipa matumaini huenda amebadilika, na anapoiona no yake ya simu lazima moyo unaenda mbio,. Hii ninayoisema ilishanitokea.
   
 10. miss wa kinyaru

  miss wa kinyaru JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 543
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyo mwanaume wala hana mapenzi tena, aachane nae, tena mwambie afute no yake ya simu kabisa ili aachane na mawasiliano, akipigiwa amuulize nani mwezangu, akimuuliza mara mbili hatapiga tena, na yeye itamsaidia kusahau taratibu,kwasababu anapopigiwa ndio kidonda kinatoneshwa na kujipa matumaini huenda amebadilika, na anapoiona no yake ya simu lazima moyo unaenda mbio,. na kila simu inayoingia kwake lazima ashituke anahisi labda ni yeye kampigia. Hii ninayoisema ilishanitokea.
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hakuna desa la summary pale contena?
   
 12. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kwanza hebu jifunze kupanga aya na kama vp summary ni muhimu..kumbuka unawaandikia Watanzania.
  Baki tu ze topiki..nadhani huyu ndugu..(japo nahisi ni wewe) mwambie awe na subira na awe na upendo usio na matarajio makubwa..wanaume tumebaki wachache wengi ni wavulana.
  Ni hayo tu!
   
 13. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,365
  Likes Received: 981
  Trophy Points: 280
  Mwambie aje huku jf,wanaume wa huku wako very serious kwenye mapenzi.
   
Loading...