USHAURI: Si lazima ufe mwana CCM!

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Nimepata kusikia baadhi ya wazee hasa wapenda mabadiliko ambao ni wakereketwa wa CCM wakisimulia jinsi Baba wa Taifa, Hayati J.K Nyerere ambavyo alipata kumkemea hadharani, rafiki yake kipenzi; KAWAWA baada ya kutoa ahadi nzito ya kufa mwana CCM siku moja wakiwa dodoma! Nyerere alimwambia ilikuwa si busara kwa KAWAWA kuahidi ahadi nzito kwa chama kilichozikwa na azimio la ZANZIBAR! Wito wangu kwa walio na mtazamo kuwa CCM ipo kwa ajili ya kutawala milele, ni vema mukaamini kuwa sasa imekwisha!

Badilisheni mtazamo na mkubali kushindwa! Tofauti zetu za kisiasa zisitugawe! Ukiona kwangu kuzuri njoo, sote ni ndugu! Haina maana kufia sehemu mbaya wakati ungeenda kwa jirani ungepewa msaada na kuendelee kung'aa! Hizo kadi ni makaratasi tuu! Watu huhama dini zao sembuse chama!! KARIBUNI , CHADEMA tu-reconstruct taifa letu! Ila huku kwetu kuna masharti madogo madogo tutawapa na mkubali kuyafuata! KARIBUNI SANA!
 
Back
Top Bottom