Ushauri Pekee kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Ushauri Pekee kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

enery

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2015
Posts
368
Reaction score
439
National Housing wamejitahidi sana kujenga nyumba zenye ubora sehemu mbalimbali ndani ya nchi yetu katika mikoa mbalimbali lakini nyumba hizi zimekuwa zikikaa bila wapangaji wala wanunuzi kwa muda sasa, nimepita Mkuranga naona nyumba zipo tu, Kihonda mkoni morogoro hali kadhalika hata Iyumbu dodoma na kwingine kwinginkama Kigoma, Katavi, Shinyanga n.k. Bei ya nyumba izi kwa kipato cha mtanzania kipo juu kwa sasa na ndo mana watu wanakuwa wazito kuzinunua. Je nini kifanyike? Kuna vijana wengi sana wanafanya kazi kwa sasa, hivi nyumba wauzieni kwa mkataba wa malipo ya kila mwisho wa mwezi kama mpangaji hata kwa miaka 10 ama 20 kijana anaweza kukilipa kila mwisho wa mwezi. Mfano nyumba ya Milioni 45 ukimpa kijana kwa miaka 10 au 20 ataitunza kwa kuwa anajua mwisho wa siku itakuwa yake na familia yake. Miaka 20 ni sawa na miezi 240 ukichukua Milioni 45 ukagawa kwa miezi 240 utapata tshs 187,500/= hiki ni kiasi ambacho kijana anakimudu. 45,000,000/240=187,500 kiasi hiki kinalipika na mtu atakuwa na moyo wa kulipa kwa kuwa anajua mwisho wa siku nyumba itakuwa yake, asipolipa anajua kuwa malipo aliyokwisha fanya yatakuwa yaneenda bure hivyo kijana atafanya juhudi kulipia nyumba yake. Kwa kufanya hivi Shirika litapata fedha za kutosha kila mwezi pia wataweza fanya miradi mingine mikubwa kwa kuwa fedha zitakuwa zinaingia kila mwezi. Huo ndo ushauri wangu sijui kama niko sahihi ama laah waweza chukua wazo langu na kuliboresha zaidi kuliko kuacha nyumba zikichakaa bila kuwa na mtu wa kuiangalia?Naomba kuwasilisha
 
Umeongea point sana at least watu watamiliki nyumba kwa miaka ijayo na wao pia watapata profits
 
Hizo nyumba kutopata wateja ni Serikali kukosa Kiranja wa kufanya maamuzi Magumu tu. Maamuzi yawe kwamba Viongozi wote wa Serikali waliopo eneo lenye nyumba za NHC, HAKUNA KULIPWA POSHO YA NYUMBA BALI WAISHI KWENYE NYUMBA ZA NHC na Posho zao za Nyumba Hazina azielekeze NHC full stop. Hizo nyumba zitakuwa na manufaa na zitaipunguzia Mzigo Serikali kulipa posho kuuubwa za nyumba kwa Viongozi wake.
 
Back
Top Bottom