Ushauri nini cha kuzingatia unaponunua Iphone used?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
242
1,000
Naomba msaada,

Mimi ni mtundu wa android ila ios sina ujanja kabisa sababu hua sio shabiki wa ios, sasa kuna mtu kaniamini kanipa hela anahitaji nikamchukulie, sitaki kumuangusha.

Mara nyingi nasikia wengi wakilalamikia sijui Apple ID, kama sikosei wanasema waweza uchukue baadae inahitaji uifungue inasumbua,
hiki ndio hasa nahitaji kujua.

Haya yafuatayo nayajua hivyo nishauri nje ya hapa.
Refurb,
Mtumba,
Battery health

Kama kuna cha muhimu sijakitaja naomba pia msaada.
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
6,628
2,000
USINUNUE IPHONE USED

Ukinunua kwa mtu unaemfahamu:

(1) Hakikisha una sign in kwa your own Apple ID. Yaani reset (network reset) uanze upya kila kitu.

(2)Akianza kuleta zile story za tumia Account hii hii achana nayo.

If possible nunua tu mpya mkuu.

Maana cheap is expensive. Ukiona mfano X unauziwa below 800 shtuka au 11 bellow 1.5 shtuka, au 8 below 600 shtuka.

Utaja kamatwa na unaulizwa mwili wa marehemu upo wapi?
 

Okoth p'Bitek

JF-Expert Member
Jan 11, 2019
828
1,000
IMG_1159.jpg


Inabidi sasa uhakikishe amesign out ili na wewe uweze kuregister apple id yako
Ndio utaitumia kwenye appstore itunes na issue nyingine

Kuhusu battery health ukipata kuanzia 85 sio mbaya
 

recycle Bin

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
3,121
2,000
1 hakikisha Apple ID ya anaekuuzia simu anaitoa kuruhusu wewe kuweka/kutengeneza ID yako.

2 Hata kama unayo apple ID jaribu kufanya kama you are new ucreate New ID lengo ni kubaini kama simu imetumika sana. Hapa ikiwa zaidi ya Users 3-5(sina hakika sana) huwa inakataa kucreate new Id. Hii ni mbaya baadae ukitaka kuiuza itabidi uiuze kwa mtu mwenye apple Id au uache Id yako aitumie.

3 Battery health isishuke 85%

4 hakikisha haina crakes kwenye screen

5 Hakikisha simu umeikagua mwenyewe au kama ni mkoan basi ukaguz mtumie mtu unaeamin anazijua iphone na unamjua vizuri.
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,817
2,000
niliokota iphone, tangu ikiwa on mpaka imezima yenyewe na uzuri kulitumwa msg ya tigo pesa kupitia line iliokuwemo humo imetumiwa laki moja

ipo kabatini tu sim nzuri lakini ina bonge la password nina kazi ya kuitoa na kuirudisha niliikuta na missed call mpaka imezima sjui mwenye nayo ni nani ni muda mrefu mno kuitupa nashindwa kuitumia nashindwa
 

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
2,784
2,000
nimeokota iphone, tangu ikiwa on mpaka imezima yenyewe na uzuri kulitumwa msg ya tigo pesa kupitia line iliokuwemo humo imetumiwa laki moja

ipo kabatini tu sim nzuri lakini ina bonge la password nina kazi ya kuitoa na kuirudisha niliikuta na missed call mpaka imezima sjui mwenye nayo ni nani ni muda mrefu mno kuitupa nashindwa kuitumia nashindwa
Iphone aina gani?
 

DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,079
2,000
Naomba msaada,
Mimi ni mtundu wa android ila ios sina ujanja kabisa sababu hua sio shabiki wa ios, sasa kuna mtu kaniamini kanipa hela anahitaji nikamchukulie, sitaki kumuangusha...
Hivi iPhone zina maajabu gani? Nitoeni ushamba...
 

recycle Bin

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
3,121
2,000
niliokota iphone, tangu ikiwa on mpaka imezima yenyewe na uzuri kulitumwa msg ya tigo pesa kupitia line iliokuwemo humo imetumiwa laki moja

ipo kabatini tu sim nzuri lakini ina bonge la password nina kazi ya kuitoa na kuirudisha niliikuta na missed call mpaka imezima sjui mwenye nayo ni nani ni muda mrefu mno kuitupa nashindwa kuitumia nashindwa

Upo wapi? Nna jamaa yangu alipoteza iphone yake 6s ni mda sasa umepita
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom