Ushauri: Nifanyaje niwe na huyu msichana bila kumuudhi msichana wa zamani

lavian

JF-Expert Member
Jul 13, 2015
722
329
Kwanza kabisa harakati za maisha zinaendaje wakuu,

Kilicho nifanya nije apa mbele yenu kuomba ushauri ni kuwa, juzijuzi tu baada ya kuachana na mschana wangu ikanibidi nitafute wa kupotezea mda mpaka nitakapoona wa kumpenda, kweli nikampata fasta tu nikawa nae, baada ya siku chache nikakutana na msichana kitaa nikajua huyu ndo wa kukaa nae mda mrefu maake alikuwa amekidhi vigezo vyote ninavyoviitaji.

Nikamvutia pumzi, siku flani hivi nikaja kumuona yule poteza mda wangu yule yuko pamoja na yule niliegundua nikiwa nae nitadumu nae, nikapita kwa kujificha maana sikutaka wanijue na kisha kuharibu mipango yangu ya PROJECT GET, baadae kuja kumuuliza yule mpoteza mda akanambia yule ni rafiki yake sana yani kitaa akuna wa karbu kama yeye.

Wakuu nifanyeje ili niweze kuwa na yule best yake bila kuonwa mtu mbaya
Nitashukuru kwa michango yenu na wenye matusi mnakalibishwa maana ni haki yenu kuchangia na kudhani binadamu ni maroboti.
 
Hajui,ila najua ana boyfriend,nilimwambia asiachane nae kwanza
Daaaa dunia hii .... Ok ila utasababisha Kwanza huyo dada na Rafiki ake wagombane, pili lazima uonekane mbaya na ndicho hutaki.... Kwanza uhusiano wenu una muda gani?
 
Eti 'mpoteza mda',wanamume tuna tisha..!

Wachonganishe tu,Bond ikishavunjia chagua huyo unayetaka

Au mwambie ukweli tu,kwani huyo mpoteza mda ana expire lini?
 
Wanaume wengine ndio maana mambo hayatuendei vizuri, tazama huyu, kaachwa halafu badala ya kujipanga apate wa ukweli katafuta janga lingine tena. Sasa linamtesa anakuja kulialia humu
 
huwez kumuangalia msichana kimuonekano tu thn ukasema unataka awe mkeo...atleast nimejifunza icho by now
 
Yamenitoka matusi ya nguoni nilipowaza mwanangu kipenzi au mdogo wangu kuwa katika nafasi ya kupotezewa mda.
 
Daaaa dunia hii .... Ok ila utasababisha Kwanza huyo dada na Rafiki ake wagombane, pili lazima uonekane mbaya na ndicho hutaki.... Kwanza uhusiano wenu una muda gani?
Leo ni sku kama ya 9 mkuu
 
Eti 'mpoteza mda',wanamume tuna tisha..!

Wachonganishe tu,Bond ikishavunjia chagua huyo unayetaka

Au mwambie ukweli tu,kwani huyo mpoteza mda ana expire lini?
Hahaha,mkuu cjaanza ata kuongea na ninae mpnda,kuonekana kwake mtaani insue
 
Wanaume wengine ndio maana mambo hayatuendei vizuri, tazama huyu, kaachwa halafu badala ya kujipanga apate wa ukweli katafuta janga lingine tena. Sasa linamtesa anakuja kulialia humu
Mkuu mschana nilie achana nae tuna historia ndefu sana na nikimkumbuka naumia,kifupi ni kuwa unaachana na mschana af unampenda na kurudiana nae haiwezkan kabisa af kibaya zaid we ndo ulimwambia tuachane baada ya ujingaujinga wake
 
Back
Top Bottom