Ushauri: Next move ya JPM iwe katiba mpya

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
20,009
38,308
Mhola mhola..

Natumai mko salama mkitafakari na kujadili kwa umakini ripoti iliyotolewa leo juu ya makinikia, iliyolenga zaidi masuala ya kiuchomi na kisheria.

Moja kati ya mapendekezo ya kamati nikuhakikisha wote walio husika katika suala la mikataba hii iliyolitia hasara taifa, waweze kuchukuliwa hatua..baadhi ya walio tajwa ni Chenge aliyekua mwanasheria mkuu,kalamagi aliyekua waziri wa nishati n.k.

Ukitazama kwa undani suala hili kisheria mikataba hupitia na kujadiliwa na baraza la mawaziri kabla ya kupitishwa, ambapo rais, makamu wa rais ni wahusika wakuu..ukitazama kwa uhalisia katiba ina walinda hawa maraisi wasishtakiwe kwa makosa yaliyotokea kipindi cha utawala wao.

Hivyo kuwafanya wao wawae salama katika hili hata kama huenda wao walishinikiza hili kwa masilai fulani fulani.

Kwanza na mpongeza JPM kwa ujasili huu mkubwa wa kulitetea taifa letu katika vita hii ya uchumi..hivyo basi kama mzalendo halisi, afufue mchakato wa katiba mpya utakao linda masilahi ya taifa hata kama yeye akiondoka..inchi iendelee kuwa katika misingi bora ya kizalendo kama alivyotuonyesha.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom