Ushauri: Nataka kuweka advance ili ninunue nyumba.

Ushauri: Nataka kuweka advance ili ninunue nyumba.

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,474
Habari za majukumu wakubwa na wadogo.

Adhima ya kuleta uzi huu ni kutaka kupata ushauri kutoka kwenu..
Moja kwa moja kwenye mada.

Asilimia kubwa humu najua wamepitia kipindi kigumu cha maisha ya kupanga na mpaka leo kuna wenzangu bado wamepanga kama mimi. Kuna changamoto ambazo tunakutana nazo kwenye majumba ya kupanga mpaka unatamani ardhi ipasuke.

Maana yangu...

Mimi kutokana na kero za kukaa kwenye nyumba za kupanga nimeamua rasmi mwisho wa mwezi wa tisa mwaka huu ninunue nyumba ambayo bei yake ni milioni 25..

Sasa basi, pamoja na yote, nyumba hiyo nimeipenda sana na pia nimejaribu kuzungumza na kaka wa mwenye nyumba kwamba aniekee hadi mwezi huo kakubali..

Lakini hata hivo.. Kasema ikiwa naitaka nimpe japo advance japo milioni 5 ili awe na uhakika wa kwamba naitaka.
Kwa bahati mbaya kwenye account similiki hizo bali kuna 3.5 na ndizo ambazo nimepanga kuja kumpa lakini kwa masharti na ndio lengo la kuleta uzi wangu hapa.

Kwenye nyumba kuna kaka mtu ambae anakaa mpaka nyumba ipate mteja ili baadae akahamie kwenye nyumba yake, sasa nimepanga kumwambia kwamba aniachie mimi hiyo nyumba mpaka mwezi tuliokubaliana kwa kuepuka kero la nyumba za kupanga lakini sijamwambia.

Wasi wasi wangu ni kuja kukataa hicho ambacho nataka kumuomba.. Ifahamike kwamba yeye ana nyumba yake japo anakaa kwa Dada yake mpaka iuzwe...

Ushauri kutoka kwenu... Je nimuanze vipi ili akubaliane na mimi? Maana nahisi kama itakua tofauti na matarajio yangu. Au kabla ya kumpa pesa nimwambie akikataa nikatafute nyengine ambayo mwenye nyumba anaweza kunikubalia ombi langu???
 
Back
Top Bottom