Ushauri: Namwombaje msamaha huyu mtu?

Ushauri: Namwombaje msamaha huyu mtu?

Aisee kama sijakosea siombi msamaha,hata awe nani.nlishafukuzwa shule sababu hiyo.nikikuomba msamaha ujue nimemaanisha kutoka moyoni na nlikukosea kweli,si vinginevyo.
 
Vitoto vya dot.com vina shida sana, unaleta dharau wakati umekalia kuti kavu. Unakata simu ili iweje? Kakupigia tena haujapokea, baki na hasira zako sasa. Unafikiri kulipia mtu ada mchezo!.

Mpigie simu muombe msamaha. Unaweza kumwambia ulikuwa umetoka kuadhibiwa kwa kosa usilolifanya kwahiyo haukuwa katika mpangilio mzuri wa kimawazo ,lakini jirekebishe
Wewe nae wale wale tu... Kumlipia mtu ada unaona kama kumnunulia mtu meli vile!! Kikubwa kuheshimiana tu kwani ada kitu gani bana
 
Aisee kama sijakosea siombi msamaha,hata awe nani,nlishafukuzwa shule sababu ,hiyo.nikikuomba msamaha ujue nimemaanisha kutoka moyoni na nlikosea kweli,si vinginevyo.
Dah! Kweli aisee .. Kwa mwandiko huo ni kweli ulifukuzwa shule! Mi sijakukosea ila samahani kwa kukuambia ukweli
 
Habari....

wakuu leo asubuhi kuna mtu alinipigia simu ni ndugu ninayemtegemea kwenye masomo akawa analalamika kwa baadhi ya mambo ambayo sio sahihi nimefanya ilipofika sasa point ya kunifanisha na jinsia tofauti..sikutaka mjadala nikakata simu hapo hapo....

-Sasa hii imekuwa kesi kubwa ambayo hata sikutarajia mimi mwenyewe na hasira ila kwa kuwa yeye ana mamlaka nimeamua nimuombe msamaha...

Sasa najiuliza naingia kwa gia gani??niandike sms yaishe...??au nimpigie simu sasa kwenye simu hapa ni muongeaji sana??
Pole ila utakua umejifunza,haijalishi awe anakulipia ada au hakulipii ila heshima ni kitu cha bure,JF utasikia mengi wengine watakupa ushauri wa achana nae na wengine wataku advice vyema ila mwisho wa siku wewe ndio utakae face mazuri na mabaya watakao kwambia achana nae au ningekua mimi ningefanya 1234,kubali makosa wala usijiume mpigie umuombe msamaha wacha aseme anachosema maneno hayababui,na mwenyezi mungu humpa mja wake mitihani kwa kila njia
na wala huto pata shida milele ipo siku mwenyezi Mungu atakufungulia milango ya kheir zidi kumuomba kwa nia safi na
atakujibu maombi yako, sisemi haiumi kuomba msamaha mtu wakati huna kosa ila hata mwenyezi mungu anampenda zaidi mtu anaeomba msamaha japo kosa ni sio lake..
muepushe shetani mpigie ongea nae na Inshallah mwenyezi mungu ataleta wepesi na maisha yataendelea hay ulofanya nimakosa ya kibinadamu...
 
Hata kama mtu anakusaidia asikunyanyase na wewe kuwa na jeuri, tena mpigie mwambie nimekukatia simu makusudi kwa sababu hukupenda alivyo kutusi na wewe mchane live, haya majsha yapo tu mambo ya kutishiana na kunyanyasana ni zamani sio sasa hivi.

aiseeee I wish ningekuwa mimi hapo yeye ndio angekuwa ananiomba msamaha.
safi sana,unajitambua sana.
 
Back
Top Bottom