Ushauri na utayari katika mambo ya usalama

Status
Not open for further replies.

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Jamani si kwamba nimehisi tishio lolote la hatari la kiusalama nchini kwetu.


Leo nimeona na kusikiliza katika CNN wenzetu (USA) wakidadavua mjadala kama mfumo wao wa rangi wa kushauri hali ya usalama kwa wananchi na asasi zote bado unafaa.

Maswali:
1. Je sisi tuna mfumo gani wa kuwajulisha wananchi wakati wa janga dhanio lolote la kiusalama ili kila mwananchi awe tayari katika kuchukuwa hatua zinazopaswa pindi tapatapo kielekezo fulani?

2. Kama tunao mfumo fulani, je wananchi walio wengi wanaufahamu na ubora wake ukoje

4. Kama unafikiri hatuna tufanye nini

Hapa chini unaweza kuona Marekani wanavyotumia rangi kumaanisha hali tofauti ya usalama.


amd_homeland_security_terror_levels.jpg
 
Rangi bongo!!!

Mkuu hapa ni luitisha mkutano na waandishi wa habari, ukiongozanan na makamanda wa majeshi yetu, period!!!

Hii naona kama haiwezekani kwetu!! Maana inaidi ilmu itolewe kwa kiasi kikubwa maana ya rangi hizi. Watawala wetu hawako tayari kwa hili, kwani si kipaumbele kwa sasa!!! Watoto wetu wenyewe wanakaa kwenye mawe wakiwa darasani, watajua lini?:hand:
 
Sisi tunajishuhulisha na maswala ya Ugali na maharage kwanza , hapo tutakapokuwa tumeshiba hayo mambo ya rangi [ hali ya usalama] pengine ndiyo yatakuwa relevant!! Ukiwa na njaa hayo mambo ya usalama hayana kipaumbele katika maisha yako kwani priority yako inakuwa survival yako as a human being.
 
Tusibeze yasiyobezeka. Suala la usalama ni kuntu na inapaswa kweli jamii na mamlaka kukaa chini na kutatua tatizo la danger alert. Linapokuja suala la rangi naunga mkono kwa kuwa sio wote wanajua kusoma na kuandika (shame on CCM) lakini wanaoona na wanaweza kufundishika kuhusu alama au rangi za hatari.
USALAMA ni kipaumbele cha kwanza kwa kuwa kama jamii haiko salama hakuna plans za maendeleo zitakazofanikiwa wala kupangwa
Tatizo ni pale wabongo wataapotaka kuzitumia alama za rangi kuainisha maeneo yenye ujambazi au tukio la ujambazi.......
 
Kuna usalama bongo zaidi ya kuhangaikia matumbo yetu kwanza??
 
Ukiona FFU wanapasha ujue ndio hiyo nyekundu ya kimarekani. Hapo inabidi ulale mbele kwa sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom