Ushauri na mambo ya kuzingatia kwa DC Polepole, Musoma yetu

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,633
2,297
Mheshimiwa polepole hongera kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Musoma. Musoma hatuna matatizo mengi ila zaidi ni ukarimu kwa wenyeji, na kushirikiana bega kwa bega kwenye maendeleo.

Ila nakushauri, ukifika shughulikia yafuatayo kwa ukaribu:-

i) Mradi wa maji ambao hauna dalili zozote za kukamilika mpaka sasa. Wananchi wanapigwa kalenda kuliko kukicha.

ii) Fuatilia kwa karibu miradi inayoendeshwa na manispaa hasa miradi ya barabara inayofadhiliwa na benki ya Dunia.

iii) Fuatilia pesa ya SACCOS tulio ahidiwa lkni imeliwa na wajanja wa manispaa tsh 30M.

Iv) Fuatilia kero za watumishi wa Musoma, maana kama zinaongezeka hasa kwa kutopandishwa vyeo bila sababu yoyote ya msingi.

v) Hospital ya wilaya ya Nyasho ina matatizo ya kudumu

vi) Fuatilia gharama za walinzi wawili wa kampuni binafsi wanaolinda kwa mkurugenzi ni gharama za nani

vii) Fuatilia customer charge ya kila mwisho wa mwezi inayotozwa na idara ya maji wkti huduma ya maji haipatikani muda wote.

Tunakutakia utekelezaji mwema.
 
Musoma mna hasira subirini kwanza mheshimiwa afanye part ya kujipongeza na kukata keki...
 
Nilisahau pia Mheshimiwa, ukumbuke na vile vifaili vyetu kule TAKUKURU, maana vifaili huko vipo vingi.
 
Combination yake na Mulugo mkuu wa mkoa ukijumlisha na Matayo mbunge UKAWA jimbo walisahau kwa muda
 
Ndio mkuu labda tuone hii slogan inaweza kutufukisha mahali..
Kwa kipindi hiki kifupi inaonekana Kuzaa matunda ya hapa na pale ingawa changamoto haziwezi kosekana cha msingi nikuangalia namna nzuri yakuzishughurikia.
 
Tunamsubiri kwa hamu sana. Maana bado kijana, na tuone anaendana na falsafa ya hapa kazi tu?
 
Majukumu ya nafasi za viongozi yanaingiliana sana kwa Tanzania. Hebu fikiria kuna diwani, mbunge,mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa. Unaweza ukanipa wapi huyu anatakiwa afanye, huyu asifanye
 
Pia Mheshimiwa usiwaze sana kuja huku eti watu wanasema utakuwa unakosekana kwenye media. Sasa hivi kuna usafiri wa ndege aina ya precision air inakuja mara mbili kwa wiki. Hivyo tunaamini kwenye media channel ten kama kawa
 
Back
Top Bottom