Ushauri: Mwanasheria Mkuu alazimishwe na bunge kutoa muhtasari wa kesi zote dhidi ya Tanzania

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,684
Nashauri bunge limlazimishe mwanasheria mkuu atoe muhtasari wa kesi zote,ndani na nje ya nchi ambazo tumeshtakiwa,na jumla ya kiwango cha madeni yaliyothibitishwa na mahakama na yale yanayosubiri kuthibitishwa na mahakama,na kwa ufupi chanzo cha madeni hayo

Taarifa hiyo isomwe tu kama taarifa,na bunge lisiijadili

Kwa sasa inaonekana kesi hizi ni kichaka cha kuifilisi nchi
 
mmmmh!!! siku hiyo patachimbika. Najua serikali itakataaa
 
Kama kusema tu ni jinai, hilo halitawezekana jo! Wanatamani wangekuwa na uwezo wa kublackout kabisa vyombo vya habari hususani Internet wangefanya hivyo ili kila kitu kisijulikane!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Binadamu Wajinga Sanaa.. Eti Wako Huku Mtaani Kwetu Wanashangiliaa Eti JPM komoa Hao Matajiri Waishi Kama Sisi... Sasa Najiuliza Hao Matajiri Sindio Wameajiri Watoto Wao, Ambao Kwao Wanategemea Kupata Mkate Wa Ahsubuhi.. Pooor Tanzani Poooorr.. Shame On You Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mmmmh!!! siku hiyo patachimbika. Najua serikali itakataaa
Hii ni sehemu ambayo imejificha,wananchi wanakuja kustukia kesi imeisha na tumepigwa,lakini kama mwanasheria mkuu akiwa na utaratibu wa kutoa ripoti bungeni,itasaidia kuisimamia serikali na pia hata wale wanaovunja mikataba ovyoovyo au ambao wanafanya watajizuia wakijua kwamba bunge litataarifiwa
 
Heeeeeeeeeeeeeeeeee uko wapi kama kumkosoa rais hadharani ni kosa je kutamka tunadaiwa bei flani hili si ni JINAI?
 
Nashauri bunge limlazimishe mwanasheria mkuu atoe muhtasari wa kesi zote,ndani na nje ya nchi ambazo tumeshtakiwa,na jumla ya kiwango cha madeni yaliyothibitishwa na mahakama na yale yanayosubiri kuthibitishwa na mahakama,na kwa ufupi chanzo cha madeni hayo
Mbona taarifa kama hii unaweza kuipata hata TLS?wala haina haja ya kuilazimisha serikali,ni kwa kua wengi hamfuatilii tu habari za serikali.
Ungesema pia serikali ikupe taarifa ya wadaiwa sugu wa kodi ambazo wamekata rufaa baraza la kodi Tax Tribunal kwa miaka kumi sasa serikali inadai jumla ya kodi ya Tsh.Trilioni 3 kwa wafanyabiashara mbali mbali sijui kama unalijua hilo
 
naunga mkono hii hoja..
ni vizuri taifa likawa na takwimu sahihi na sio kuishi kimazoea pasipo kujua ukweli..
 
Nashauri bunge limlazimishe mwanasheria mkuu atoe muhtasari wa kesi zote,ndani na nje ya nchi ambazo tumeshtakiwa,na jumla ya kiwango cha madeni yaliyothibitishwa na mahakama na yale yanayosubiri kuthibitishwa na mahakama,na kwa ufupi chanzo cha madeni hayo

Taarifa hiyo isomwe tu kama taarifa,na bunge lisiijadili

Kwa sasa inaonekana kesi hizi ni kichaka cha kuifilisi nchi
Kiutaratibu hayo yote huwekwa wazi na kushughurikiwa ndani ya vikao vya baraza la mawaziri ambalo ndilo lina act kama executive committee ya muhimili wa serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona taarifa kama hii unaweza kuipata hata TLS?wala haina haja ya kuilazimisha serikali,ni kwa kua wengi hamfuatilii tu habari za serikali.
Ungesema pia serikali ikupe taarifa ya wadaiwa sugu wa kodi ambazo wamekata rufaa baraza la kodi Tax Tribunal kwa miaka kumi sasa serikali inadai jumla ya kodi ya Tsh.Trilioni 3 kwa wafanyabiashara mbali mbali sijui kama unalijua hilo
Watanzania hawakuipigia kura TLS iongoze nchi
 
Hii ni sehemu ambayo imejificha,wananchi wanakuja kustukia kesi imeisha na tumepigwa,lakini kama mwanasheria mkuu akiwa na utaratibu wa kutoa ripoti bungeni,itasaidia kuisimamia serikali na pia hata wale wanaovunja mikataba ovyoovyo au ambao wanafanya watajizuia wakijua kwamba bunge litataarifiwa

Mkuu ni hivi kwa sasa hakuna bunge linaloisimamia serekali, bali ni serekali ndio inalishauri na kulisimamia bunge. Huoni Spika anafanya kila analoambiwa na rais, na hata utendaji wake ni wakumfurahisha rais. Na sio bunge tu kuwa mateka wa serekali; baki hata mahakama ni hivyohivyo.
 
Back
Top Bottom