Ushauri muhimu wa kibiashara kwa Form Four waliomaliza

Naja naja

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
747
1,452
Kwa vijana waliomaliza Form Four mwaka huu wanaosubiri matokeo yao ninawashauri wakati huu mkiwa mpo tu nyumbani mnasubiri majibu ya matokeo yenu, nendeni mkajifunze ufundi wa kompyuta na simu haswa upande wa software.

Ujuzi huu utawasaidia sana mkifika chuo, kamwe hamtokaa msubirie pesa ya boom ili muishi kulingana na mahitaji yenu.

Ukiwa fundi wa kompyuta na simu, kuingiza zaidi ya elfu 50 kwa siku ni kawaida sana.

Wateja wa simu na kompyuta ni wa uhakika sana maana hivyo vitu ni muhimu sana kwenye maisha yao, vitu kama nguo, radio, friji, TV nk ni kawaida sana mteja kukuletea kisha anavitelekeza vitu vyake, ila wateja wa simu na kompyuta hao ni uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom