Ushauri Msaada wandugu

Enny

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
962
Reaction score
131
Nimepata kazi sehemu mbili kwa wakati mmoja. Moja ni kwenye private company ya nje ndio inataka kuanza kazi nchini. na ofisi itakuwa hapa Dar es Salaam.

Nyingine ni kwenye shirika la umma lakini kazi ni mkoani ingawa likizo itakuwepo baada ya mwezi na nusu , likizo siku ishirini. Kuhusu mshahara sehemu zote unalingana.

Nimeshindwa kuamua niende wapi kati ya hizo sehemu mbili.
 
Nenda serikalini
hata kama kituo cha kaz kingekua gereza la Keko au Ukonga
 
Asante Nashukuru kwa ushauri wako
 
Hapa dsm una miradi yoyote unayosimamia? Kama huna lolote hapa mjini nenda serikalini it could be da best for your future
 
Sina mradi wowote ninaosimamia ila familia ipo Dar
 
Asanteni wote mlionishauri na kuchukulia swali langu seriously Mungu wabariki sana
 
Sina mradi wowote ninaosimamia ila familia ipo Dar

Familia unamaanisha nini mpendwa? mme/mke na watoto? Kama ni hao, nakuambia hivi, long distance relationship haiwork. Kama unampenda mkeo/mmeo usiende mbali nae.

Nimesema mimi babu ODM
 
Nakushauri xana ndugu yangu nenda serikalin tu ndg kwasababu utakuwa na uhakika wa maisha yako ya baadae.Kwa nn nasema ivo ilo shilika ambalo linaanza hapa tz likifilisika ol waka amua kufanya downsizing of workers after backrupt utafanya nn!??bora serikalin bhana fanya ivo kwa manufaa yako na familia yako ya baadae mtanzania mwenzangu.
 
Asanteni wote kwa ushauri nimeamua kwenda serikalini sasa
 
Mwaya nenda serikalini,familia ipo tu na hivyo kuna likizo shaka ondoa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…