Ushauri: Mke wangu anatembea na mfanyakazi mwenzie hadi kamzalisha

Mpaka nimeamua kukuandika sijui nifanye nini, mimi ni kijana wa miaka 33 nimeoa na nina mtoto mmoja na sasa hivi mke wangu amekwenda nyumbani kwetu kujifungua na hii ndio sababu ya mimi kuja kukuandikia.

Iko hivi, mimi na mke wangu tulikuwa vizuri sana katika ndoa yetu, ni mwanamke ambaye niliona ananiheshimu na kujali kweli kila mtu anampenda. Hatujawahi kugombana lakini wiki mbili zilizopita alikwenda kujifungua nyumbani kwetu, mimi ndiyo nilimpeleka lakini kurudi nyumbani katika kuhangaika kufanya usafi ndiyo nikakuta kuwa kuna laini ya simu ambayo ilikuwa kama imedondoka.

Nilipanga kuitupa ila nikaamua kuiweka kwenye simu kuangalia. Sikukuta kitu cha maana hivyo nikaamua kuitoa ila kabla ya kuitoa kuna SMS Mbili ziliingia ni kama zile zinasubiri uwashe simu ndiyo ziingie.

Ni meseji za mwanaume ambaye alikuwa akilaumu mke wangu kwa kwenda kwetu kujifungua. Kuna SMS moja ndiyo uliniumiza zaidi, uliandikwa “Mtoto wa kwanza nilihudumia mimba unajifungua mtoto kafanana na huyo mwanaume wako! Huyu wa pili nimekuambia anataka niwe karibu na wewe umeenda kujifungulia kwenu?

Nataka ujue kwamba huyo mtoto kama ni wangu ukirudi namchukua sitaki mwanangu kuishi na huyo Boya!”

Niliiangalia ile namba nikaja kugundua kwamba ni namba ya mfanyakazi mwenzake, nikafuatilia mtandaoni nikajua ni mtu ambaye namfahamu hata kwenye harusi yetu alikuja huyo kaka na wafanyakazi wenzake tena kama familia yake hata ile kutafuta hoteli kwa ajili ya wageni nilitafuta mimi na huyo ni mmoja wao wale ambao alitoa list ya watu wake watakaokuja siku ya harusi.

Sikujibu chochote hizi meseji na mpaka sasa hivi hakijatumwa chochote, nahisi labda mke wangu kamwambia kuwa hiyo laini kashapoteza sijui, ila ninachowaza sasa hivi nifanye nini? Nimekaa na hiki kitu wiki mbili mwenyewe nahisi kuchanganyikiwa kweli najiona kabsai nafanya vitu ambavyo sivyo naomba ushauri nifanye nini?
Mfowardie yeye na hawara yake hiyo meseji kutokea kwenye simu yako halafu kausha
 
Nina wasiwasi na hilo. Ungekuwa unampenda bado usingemuanika hapa jamvini. Ungegugumia tu na machungu yako. Halafu huko mbeleni kwa vile yule jamaa naye anampenda sana kiasi cha kukuita wewe kuwa ni Boya ni yale ya mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi. Tahadhari kabla ya hatari.
Ni kawaida
 
Mkuu tulia kwanza! Usifanye papara,wala usipanic! Tunza hizo sms! subiri mkeo ajifungue.
 
Dogo Hii ni habari ya kweli au umetunga??? Ili tukushauri kwa uhalisia kama umetunga huu mwezi mtukufu utalaniwa. KAMA NI KWELI sema ni Kweli.
 
Back
Top Bottom