Kwanza napenda kukupongeza kwa kuteuliwa tena kuwa Waziri wa Ardhi. Natambua moja ya matatizo makubwa ya wananchi ni kuwa na makazi bora. Napenda kutoa ushauri ufuatao kwa utekelezaji zaidi:
1. NHC inafanya kazi kubwa sana katika kujenga makazi na majengo ya biashara nchini. Hata hivyo mimi binafsi sioni kama makazi hayo yanamsaidia mwananchi wa chini kwakuwa hawawezi kumudu kununua nyumba hizo (ikizingatiwa mnatumbua majipu sasa hivi). Hivyo, nashauri uanzishe utaratibu wa kuwezesha shirika kujenga nyumba na kupangisha wananchi kwa mkataba kuwa baada ya miaka kadhaa mwananchi anapewa haki ya kumiliki nyumba.
Hii ni sawa na vile ambavyo sasa hivi wanakopeshwa na mabenki na kulipa kwa miaka 20. Mtakuwa mmesaidia wananchi kwa kiasi kikubwa kumiliki nyumba kwa utaratibu nafuu na rahisi. Hii inafanyika kwa nchi baadhi za Middle East.
2. Katika awamu yako ya mwisho ya serikali iliyopita ulizunguka nchini na kupokea kero mbalimbali kuhusu ardhi na fidia. Nyingi hazijafanyiwa kazi. Hivyo, nakuomba uanze kuzifanyia kazi ikiwemo ile ya wananchi wa Gezaulole Kigamboni, Dar es Salaam kutolipwa fidia za nyumba zao zinazopitiwa na barabara ya mita 60 kwa takribani miaka 5 sasa.
Nakutakia kazi njema. Yangu ni hayo naamini wadau wataboresha au kuongeza mengine.