Nyanje
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 495
- 376
Wataalam nina tatizo la kutoa shahawa zenye mchanganyiko na damu. Tatizo hili limenianza siku ya pili na ni mara ya kwanza.
Kabla sikuwahi kupata tatizo hili hata nipige goli tatu.
Nini tatizo na madhara ya hiyo hali.
Nawasilisha.
Maswali yenye mfanano
--
Mrejesho kutoka kwa mwalidebe
Kabla sikuwahi kupata tatizo hili hata nipige goli tatu.
Nini tatizo na madhara ya hiyo hali.
Nawasilisha.
Maswali yenye mfanano
Hivi mtu ukipiga bao na lile bao likawa kimechanganyikana na damu.Je, huu ni ugonjwa gani?
Kwa kifupi nimefanya majaribio kwa kupiga punyeto alafu cha kushangaza sina maumivu yoyote.
Wakuu naombeni msaada na nikienda haja ndogo sipati maumivu yoyote.
Naombeni maelezo wakuu.
Ndugu zangu,
Nimemaliza kufanya tendo la ndoa, lakini cha ajabu hizi shahawa zangu zimetoka na damu, hali hii imeniogopesha kuendelea na tendo la ndoa.
Ndugu zangu je hii hali ya shahawa kutoka na damu ni hali ya kawaida au nitakuwa na tatizo? Bao la kwanza hali ilikuwa hivihivi bao la pili hali bado ni vilevile yaani unaona shahawa lakini zinadamu mbichi kabisa.
Msaada ndugu zangu wa mawazo ushauri tafadhari maana huyu mwanamke niliye naye ningekuwa simfahamu ningesema labda nimekutana na jini.
--
Mrejesho kutoka kwa mwalidebe
Kwanza natanguliza shukrani kwa uongozi wote wa JamiiForums kwa jinsi ambavyo mnafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha watanzania tunapata kile kinacho hitajika kwa wakati ubora na usahihi.
Pili niwashukuru wanachama wote wa JamiiForums kwa ushauri maoni yenu na maelekezo ingawa wapo wachache wananikatisha tamaa badala ya kunisaidia tatizo langu.
Ndugu zangu ilikuwa ni baada ya kukutana na mwanamke ndipo nilikugundua hali isiyo ya kawaida baada ya kuona shahawa zangu zimekuwa damu,hali hii iliniogopesha ndipo nikaja kwenu kuomba ushauri.
Baada ushauri wenu wengi wakisema nenda hospitali ukamuone daktari ni kweli nilifanya hivyo,nikaenda kumuona daktari.
Daktari alinipa tiba baada ya kufanya vipimo na kugundua nilikuwa na UTI mkali baada ya kunipa vidonge nimevitumia nikamaliza na sasa imepita karibia wiki mbili tangu nimalize vidonge.
Sasa leo imebidi nifanye tena mapenzi ili nijilizishe je nimepona? Ndugu zangu baada ya kufanya mapenzi na kutoa shahawa hali imekuwa ileile damu tu! Kwa ufupi bado tatizo liko pale pale shahawa zinatoka za damu.
Wapenda ndugu zangu naomba sana mnisaidie nini nifanye tena ilihali nimekwenda hospitali lakini bado matokeo ni yale yale shahawa zinatoka Ila zimejaa damu na damu ni nyingi kuliko hata shahawa zenyewe.
Please I need help.