Ushauri kwako Jamal Malinzi na TFF

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,470
96,019
Kwanza niwapongeze kwa mafanikio ya Serengeti Boys kwa sasa ingawa najua si ushindi wa kitaalamu sana kwa kuwa timu tuliyokutana nayo ni dhaifu sana.

Ndugu yangu Malinzi umekuwa hapo TFF kama Rais wa Ujerumani au India kwa kuwaacha watendaji wako kuwa na maamuzi na wengine wanatumia hiyo nafasi kwa maslahi yao binafsi. Leo hii mali za TFF zimekamatwa kwa kudaiwa kodi ya serikali, baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wanadai posho zao, timu kama Yanga kila siku tunasikia wanadai fedha zao lakini wewe bado umekaa kimya.

Ulichaguliwa kuiongoza TFF na siyo kuwaachia wasaidizi wako ambao sasa wanakuingiza kwenye migogoro na wapiga kura wako. Kitendo cha uongozi wa TFF kupambana na kutaka kuikomoa Simba au Yanga ni kuingia kwenye migogoro na wapiga kura wako.

Nawashauri endelezeni soka badala ya kupambana na waendeleza soka.
 
Back
Top Bottom