Ushauri kwa Zitto Kabwe: Aunganishe nguvu na Hamad Rashid

Ushauri kwa Zitto Kabwe: Aunganishe nguvu na Hamad Rashid

Wakiungana Zitto na Hamad itakuwa ni faraja kubwa sana kwa CCM,wakati CCM wanahangaika bungeni kupambana na kichwa kimoja cha Tundu Lissu,huku mitaa Zitto na akina Hamad watakuwa wakiselebuka kupambana na UKAWA.
 
Zitto Kabwe ni kijana machachari sana hasa kwenye ulingo wa kisiasa. Kwahiyo kwa ushauri wangu ajitahidi waunganishe nguvu na Hamad Rashid ili kujenga upinzani imara. Tena Zitto akichukua ushauri wangu atafanikiwa sana, kwa kuwa Zitto na Hamad Rashid wameshawahi kufanya kazi ya upinzani Bungeni pamoja, na walielewana sana.

Na vile vile hawa ni watetezi wa demokrasia kwenye vyama vyao, pia wote walifukuzwa kwenye vyama vyao kwa malengo yanayofanana.

Zitto, chukua ushauri huo kwa moyo mmoja. Mimi ni mtu wako wa karibu sana!

Kama wewe ni mtu wake wa karibu sana basi wewe ni mnafiki mkubwa,umeshindwa nini kwenda kumwambia mtu wako wa karibu,na badala yake unakuja hapa jf?
 
ADC na CUF, mapambano Zanzibar, ACT na CHADEMA mapambano bara, kweli CCM imejipanga kutumia wasaliti kuanzisha vyama vya siasa karibia uchaguzi ili wagawe kura. Kauli ya ZZK huku awali vvyama vya siasa vinavyoanzishwa wakati wa uchaguzi au karibia uchaguzi huwa vinatumiwa na watawala kugawa kura za wapinzani, je hili ni hivyo sasa kwa ACT?

Mkuu kinacho mnasa samaki kwenye ndoana ni mdomo wake,hivyo hiyo kauli ya zzk ameitimiza kwa vitendo
 
hakika wakichukua ushauri wako wa kushirikisha hivyo vyama nakumbia wanachukua dola
nawaongezea na vyama vingine
sauti ya umma
tlp
na hivi vyama vijitahidi zito kabwe awe mkuu wao wa chama

Teeeh,teeeh,na tlp? Wachumia tumbo watauana siku ya kupata ruzuku
 
hakika wakichukua ushauri wako wa kushirikisha hivyo vyama nakumbia wanachukua dola
nawaongezea na vyama vingine
sauti ya umma
tlp
na hivi vyama vijitahidi zito kabwe awe mkuu wao wa chama
Zzk na mrema wote ni mawakala hivyo hawawezi kuwa ktk zizi moja kwani kila mmoja anatafuta sifa kwa bwana mkubwa
 
Waunganishe nguvu! Mmoja ashughulike kuibomoa Chadema bara na mwingine ashughulike kuibomoa CUF Zanzibar ili kupunguza kura za ukawa! Nani kawatuma?
 
Back
Top Bottom