Ushauri kwa Zitto Kabwe: Aunganishe nguvu na Hamad Rashid

Ushauri kwa Zitto Kabwe: Aunganishe nguvu na Hamad Rashid

lendila

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
5,805
Reaction score
4,374
Zitto Kabwe ni kijana machachari sana hasa kwenye ulingo wa kisiasa. Kwahiyo kwa ushauri wangu ajitahidi waunganishe nguvu na Hamad Rashid ili kujenga upinzani imara. Tena Zitto akichukua ushauri wangu atafanikiwa sana, kwa kuwa Zitto na Hamad Rashid wameshawahi kufanya kazi ya upinzani Bungeni pamoja, na walielewana sana.

Na vile vile hawa ni watetezi wa demokrasia kwenye vyama vyao, pia wote walifukuzwa kwenye vyama vyao kwa malengo yanayofanana.

Zitto, chukua ushauri huo kwa moyo mmoja. Mimi ni mtu wako wa karibu sana!
 
ADC wanaamini kwenye ujamaa? ADC wapo Kigoma kabla ya ACT je aunde umoja kama ukawa ama waunde chama kimoja yaani wajikane waanze upya?
 
Hautafutwa... kwani ni uzi wa kuonyesha jinsi wagonjwa watakavyoungana wakiwa mahutihuti...
 
Naunga mkono hoja pia waunganishe nguvu na akina
fahmi dovutwa
peter kuga mziray
augustine mrema
john momose cheyo
hakika watatisha zaid ya ukawa
hahahahh
 
Je ni sahihi serikali kununua magari 700 ya washa washa kwa ajili ya polisi wakati huu kuendelea uchaguzi mkuu?

Ni bei gani Jumla?
 
Kama rafiki wakaribu JF umekuja fata nini usomuita ukamweleza peke yako?
 
Naunga mkono hoja pia waunganishe nguvu na akina
fahmi dovutwa
peter kuga mziray
augustine mrema
john momose cheyo
hakika watatisha zaid ya ukawa
hahahahh

hakika wakichukua ushauri wako wa kushirikisha hivyo vyama nakumbia wanachukua dola
nawaongezea na vyama vingine
sauti ya umma
tlp
na hivi vyama vijitahidi zito kabwe awe mkuu wao wa chama
 
Nasikia msaliti Shibuda naye kamunua Tadea!Wasaliti watatu hawawezi kukaa zizi moja,watasalitiana tu?
 
ADC na CUF, mapambano Zanzibar, ACT na CHADEMA mapambano bara, kweli CCM imejipanga kutumia wasaliti kuanzisha vyama vya siasa karibia uchaguzi ili wagawe kura. Kauli ya ZZK huku awali vvyama vya siasa vinavyoanzishwa wakati wa uchaguzi au karibia uchaguzi huwa vinatumiwa na watawala kugawa kura za wapinzani, je hili ni hivyo sasa kwa ACT?
 
Inategemeana na Mpango wa CCM... Agizo la Chama Tawala litazingatiwa iwapo CCM wataongeza mafungu Zaidi ...
 
Je ni sahihi serikali kununua magari 700 ya washa washa kwa ajili ya polisi wakati huu kuendelea uchaguzi mkuu?

Ni bei gani Jumla?

Ni sahihi sababu inajua haitotenda haki huoni polisi wa burundi wanavyopata tabu? Hawana vifaa
 
Zitto Kabwe ni kijana machachari sana hasa kwenye ulingo wa kisiasa. Kwahiyo kwa ushauri wangu ajitahidi waunganishe nguvu na Hamad Rashid ili kujenga upinzani imara. Tena Zitto akichukua ushauri wangu atafanikiwa sana, kwa kuwa Zitto na Hamad Rashid wameshawahi kufanya kazi ya upinzani Bungeni pamoja, na walielewana sana.

Na vile vile hawa ni watetezi wa demokrasia kwenye vyama vyao, pia wote walifukuzwa kwenye vyama vyao kwa malengo yanayofanana.

Zitto, chukua ushauri huo kwa moyo mmoja. Mimi ni mtu wako wa karibu sana!
Ushauri wako si sawa hata kidogo!!!! ACT ni kwa ajili ya kupunguza nguvu ya UKAWA Bara na ADC ni kupunguza nguvu ya ukawa Zanzibar. Sasa ukifanya hivyo itatekelezeka?!
 
mwaka huu tutashuhdia mambo mengi sana kwenye ulingo wa kisiasa
 
Ushauri mzuri sana wapinzani wa wapinzani wakiuungana watakuwa na nguvu kubwa sana ya kuwapinga UKAWA na nguvu yao inapokuwa kubwa ndivyo na posho inavyo zidi kuwa nene kutoka kwa wafadhili wao(magamba).
 
Back
Top Bottom