Ushauri kwa wanaotarajia kuomba mkopo kwa 2016/2017

Theophili

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
354
543
Ushauri kwa wanaotarajia kuomba mkopo kwa 2016/2017

Muda wowote kuanzia sasa, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itatangaza kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti yake (www.heslb.go.tz) kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Tangazo hilo litatoa mwongozo wenye maelezo ya yanayojumuisha sifa za mwombaji, vigezo vitakavyotumika, katika utoaji mikopo, muda wa kuwasilisha maombi na mambo mengine muhimu.

Hivyo, basi, ni wajibu wa waombaji mikopo watarajiwa kusoma kwa makini tangazo hilo na kujipima kama wana sifa au hapana kabla ya kufanya malipo ya ada ya maombi na kufanya maombi ya mikopo.
Wito huu unatokana na uzoefu wa miaka iliyopita ambapo waombaji walipata usumbufu usio wa lazima kutokana na kutokuwa makini kabla ya kuomba mikopo.

Kundi la kwanza ni la waombaji wasio na sifa zilizoainishwa kwenye tangazo lakini walilipa ada ya maombi, wakawasilisha maombi yao na baadae kukosa mikopo na kulalamika.

Kundi la pili ni la waombaji wenye sifa zilizoainishwa lakini hawakuwa makini na hivyo kushindwa kutimiza matakwa ya mwongozo uliotolewa.

Maombi ya mkopo wa elimu ya juu ni kama maombi ya kazi au mtihani. Kwa kazi, mwombaji anapaswa kusoma sifa zilizoanishwa na utaratibu wa kuwasilisha ombi lake. Hivyo basi, ikiwa nafasi ya kazi inahitaji msomi wa shahada ya kwanza, mtu mwenye stashahada hatakuwa na sifa ya kuomba.

Aidha, mwanafunzi akiwa kwenye chumba cha mtihani, ana wajibu wa kusoma masharti ya mtihani kabla ya kuanza kujibu maswali. Asipofanya hivyo, si ajabu akajikuta anajibu sivyo na kushindwa vibaya mtihani husika.

Mwaka jana, kwa mfano, Bodi ilipokea maombi zaidi ya 68,000 ya mikopo. Kati ya hayo, fomu za waombaji wa mikopo 7,788 zilizopokelewa na kuhakikiwa ziligundulika kuwa na upungufu na waombaji waliokosea walipata gharama za kufika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam ili kufanya marekebisho.

Fomu hizo zilikosa taarifa muhimu kama sahihi za waombaji, nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na picha za wadhamini na baadhi ya fomu za maombi kutosainiwa na waombaji wenyewe au wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama mwongozo wa uombaji mikopo unavyotaka.

Nimalizie kwa kuwasihi wadau wote, hususan watu wanaotarajia kuomba mikopo HESLB kwa mwaka wa masomo 2016/2017, kusoma kwa makini mwongozo utakaotolewa na kuuzingatia wakati wa kufanya maombi ya mkopo kuondoa usumbufu usio wa lazima.

Tuandikie: info@heslb.go.tz au tutembelee kwenye ukurasa wetu wa
 
Mleta mada, hebu nifahamishe.Form six waliofanya mitihani yao May 2016, wataomba mkopo lini?
 
naombeni ushauri mim ni mwajiriwa nimemaliza chuo mwaka juz na wakat nasoma nilijitegemea ada mwanzo mwisho sasa mwaka huu bodi hslb wameanza kunikata je nifanye nin wakat ckuomba kabsa
 
Wakuu Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu ....mwakaa huu nilijilipiaa ada lakinii naonaa miundo mbinu yangu haipo sawa na mwaka huu ninaingia mwaka wa pili cozi yangu ni BAED ninaitaji kuomba mkupo na Jee huo mkopo nitaomba kwa sifa gaNiii nitaombaa kwa registration number ya chuo au ile ya form 6 Kamaa kawaidaaa
 
Naomba kuuliza Kwa watu waliohitimu diploma wanaambatanisha copy ya chet au transcript km unaulewa mtoa uzi nijuze
 
Huo ni ushauri tu vingine subiri bodi wakitoa vigezo vyao vya mwaka 2016/2017
 
Ushauri kwa wanaotarajia kuomba mkopo kwa 2016/2017

Muda wowote kuanzia sasa, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itatangaza kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti yake (www.heslb.go.tz) kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Tangazo hilo litatoa mwongozo wenye maelezo ya yanayojumuisha sifa za mwombaji, vigezo vitakavyotumika, katika utoaji mikopo, muda wa kuwasilisha maombi na mambo mengine muhimu.

Hivyo, basi, ni wajibu wa waombaji mikopo watarajiwa kusoma kwa makini tangazo hilo na kujipima kama wana sifa au hapana kabla ya kufanya malipo ya ada ya maombi na kufanya maombi ya mikopo.
Wito huu unatokana na uzoefu wa miaka iliyopita ambapo waombaji walipata usumbufu usio wa lazima kutokana na kutokuwa makini kabla ya kuomba mikopo.

Kundi la kwanza ni la waombaji wasio na sifa zilizoainishwa kwenye tangazo lakini walilipa ada ya maombi, wakawasilisha maombi yao na baadae kukosa mikopo na kulalamika.

Kundi la pili ni la waombaji wenye sifa zilizoainishwa lakini hawakuwa makini na hivyo kushindwa kutimiza matakwa ya mwongozo uliotolewa.

Maombi ya mkopo wa elimu ya juu ni kama maombi ya kazi au mtihani. Kwa kazi, mwombaji anapaswa kusoma sifa zilizoanishwa na utaratibu wa kuwasilisha ombi lake. Hivyo basi, ikiwa nafasi ya kazi inahitaji msomi wa shahada ya kwanza, mtu mwenye stashahada hatakuwa na sifa ya kuomba.

Aidha, mwanafunzi akiwa kwenye chumba cha mtihani, ana wajibu wa kusoma masharti ya mtihani kabla ya kuanza kujibu maswali. Asipofanya hivyo, si ajabu akajikuta anajibu sivyo na kushindwa vibaya mtihani husika.

Mwaka jana, kwa mfano, Bodi ilipokea maombi zaidi ya 68,000 ya mikopo. Kati ya hayo, fomu za waombaji wa mikopo 7,788 zilizopokelewa na kuhakikiwa ziligundulika kuwa na upungufu na waombaji waliokosea walipata gharama za kufika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam ili kufanya marekebisho.

Fomu hizo zilikosa taarifa muhimu kama sahihi za waombaji, nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na picha za wadhamini na baadhi ya fomu za maombi kutosainiwa na waombaji wenyewe au wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama mwongozo wa uombaji mikopo unavyotaka.

Nimalizie kwa kuwasihi wadau wote, hususan watu wanaotarajia kuomba mikopo HESLB kwa mwaka wa masomo 2016/2017, kusoma kwa makini mwongozo utakaotolewa na kuuzingatia wakati wa kufanya maombi ya mkopo kuondoa usumbufu usio wa lazima.

Tuandikie: info@heslb.go.tz au tutembelee kwenye ukurasa wetu wa
Mtoa mada hebu nisaidie me ni mwanafunzi wa chuo niyayekosa mkopo mwaka wa kwanza sa nataka kuomba tena tatizo sikufanya mtihani wa semester ya pili ya kumalizia mwaka kwa kukosa ada je kulingana na sifa walizotoa Bodi ya Mikopo naruhusiwa kuomba mkopo naomba ushauri wako.
 
Hivi jamani hakuna kabisa mashirika au makapuni binafsi ya kutoa ufadhili wa elimu juu zaidi ya Bodi ya Mikopo asaivii ni wazi kabisa Bodi hii imeelemewa kutokana na kuongezeka kwa wahitaji wa Mikopo ni vyema taasisi,masharika binafsi yakaisaidia kada hii watu hali ya chini wanashidwa kabisa kutimiza ndoto zao kwa sababu ya kukosa ada.
 
Back
Top Bottom