belionea
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 1,052
- 914
Mwanamke mpumbavu hutafuta mafanikio ili amtawale mume wake, ili mume wake asiwe na sauti juu yake, nakwambia huko ni kujilisha upepo, hata ungemuweka mumeo chini ya miguu yako katu huwezi kukata kiu ya moyo wako na furaha ya kweli haitakuwemo ndani yako.
Tafuta mafanikio ili kuficha aibu ya mume wako, ili wakati anapokwama bado katika malango ya wakuu na mbele ya wazazi hasa wa kwako wewe mwanamke thamani yake isishuke, unaweza kumtawala kwa fedha zako lakini kamwe huwezi kuinunua furaha kwa fedha zako.
Furaha ya kweli itakuja pale tu utakapotambua nafasi yako kwenye nyumba yenu, ndio maana unalia ukiwa peke yako, ndio maana umekuwa mkali kama pilipili, sababu furaha yako ndoani haiko kwenye kumtawala mumeo bali kwenye unyenyekevu na kutambua nafasi yako.
UKITAKA KUFURAHIA NDOA YAKO USISHINDANE NA MUME WAKO. DIVINE LADIES FOR THE DIVINE NATIONS.
TUISHI KWA AKILI NA WENZI WETU"!