Ushauri kwa Wajumbe wa NEC

Ushauri kwa Wajumbe wa NEC

Tuyuku

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
3,292
Reaction score
1,935
USHAURI WANGU KWA WAJUMBE WA NEC WA CCM WANAOSHAWISHIWA KUGOMEA VIKAO ENDAPO WAGOMBEA WAO WANAOWATAKA WASIPOKUWAPO KATIKA ORODHA YA TANO BORA.

Mambo yafuatayo watambue watambatana nayo.

1 Kwa wanec ambao ni wabunge, huo ni utovu mkubwa wa nidhamu, na hata wale wanec amabao wanagombea ubunge, pia ni utovu wa nidhamu, watapatiwa barua za onyo na watashindwa kugombea, ama kusababisha majina yao kukatwa wakati wa uteuzi kwasababu taarifa zao zitakuwapo katika vikao vya kimaadili.

2 Wanec ambao wana dhamana mbalimbali za kiserikali, watambue kwamba ccm ni chama dola, na kina mkono mrefu

3 Wanec ambao ni wanasiasa tu ndani ya chama, watambue kumbukumbu zao zitabaki ndani ya maafaili na wakati wa kugombea ukifika majina yao yatakuwa ya kwanza kutiliwa mashaka.

4 Nafasi na dhamana waliyopewa ni kubwa sana katika nchi hii, warejee dhamana waliyopewa sio kwenda kuchagua mtu wao wanaomtaka, bali wawachagulie ccm mgombea, sio mgombea wa wanec, lkn pia dhamana yao ni kuwapatia watanzania rais bora.

5Wakumbuke kuwa watanzania wanataka rais aliyeibeba agenda yao, ambaye anachukia rushwa, hana makandokando, mwenye afya njema, mchapakazi, asiyelazima umma kumuhitaji, bali umma umuhitaji wenyewe, n.k

6 Kila mnec akumbuke amebeba dhamana ya watanzania, akafanye maamuzi kwa utashi wake pasipo kusikiliza mwenzie anasema nini au wale wanataka nini, ama wasifanye maamuzi kwa huruma, upendeleo ama fadhila zile.

7 Wananafasi za kichama lakini waelewe jambo wanalokwenda kulijadili ni la dola, kwahiyo yaliyojiri yameshapita, wasisahau kwamba inapofikia hatua ya kuweka dola, hakuna umaarufu, pesa wala ushawishi bali UTII BILA YA SHURTI, SIO JAMBO LA HIYARI.

Ushauri huu unatokana na taarifa zisizo rasmi zinazosambaa na kuzungumzwa kuhusu dhamira hiyo ya baadhi ya wwanec. semina hii na iwasaidie

Wanapaswa kufahamu.

1 Watashiriki mkakati ambao litakuwa ni jaribio ambalo lisilowezekana na halitafanikiwa, kwasababu ccm ni chama na chama ni kikubwa kuliko wao, mwisho wa jambo hilo watajikuta wamebaki wao peke yao na kesi yao pasipo mtu wa kuwatetea.

2 Chama kinaandaa mgombea kwaajili ya kushika dola, na ndio malengo ya chama, kushiriki kugoma kwasababu ya kupewa rushwa ama kushawishiwa au kudanganywa ni kuchafua image ya chama katika jamii ambayo ni sehemu ya kutengeneza ukakasi katika kupata ushindi mzuri, hivyo basi ni kukiuka malengo ya chama ambayo ni kupata ushindi mnono na kushika dola, jambo hili litachafua safari yao ya kisiasa kwakuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu.

3 Kamati kuu inafanyakazi kwa niaba ya nec, ni kamati waliyoiamini na kwa hakika ni kikao ambacho hakiwezi kunyima watu haki, kitasimamia haki na kuangalia taratibu zote za kikanuni, kuipinga kamati kuu ni kuonyesha kutokiamini kikao hiko, kwa mwongozo na imani ya chama chetu huo ni utovu wa nidhamu ambao utatia dosari uaminifu wa mwanachama kwa chama chake ambalo ni jambo litakaloharibu safari yake kisiasa

4 Kanuni zimeelekeza majukumu ya kila kikao, cc itapeleka majina matano na nec itapigia kura matatu na kisha mkutano mkuu kuchagua moja, kupinga taratibu za kikanuni na kuendesha migomo isiyo halali, ni uvunjifu wa kanuni ambao ni utovu wa nidhamu pia ambalo ni jambo la hatari katika safari ya kisiasa ya wahusika.

Rai yangu,

chama kimeruhusu kila mgombea kuomba ridhaa na kufata taratibu walizoelekezwa katika swala zima la ujazaji wa fomu, utatafutaji wa wadhamini na urejeshaji ambao wagombea wote walipaswa kuufuata. Sasa ni wakati wa ndugu wanec kukiachia kikao cha cc kufanya maamuzi yake na wao kusubiri kufanya ya kwao kama ilivyo kwa mkutano mkuu ambao nao wanasubiri zamu yao na kisha wananchi wote nao wana nafasi yao.

Ndg zangu wanec, msije mkaingizwa katika agenda ambayo mwisho wa siku haitakuwa na manufa yyt kwenu, siasa katika eneo la maamuzi huwa haifanywi tena kwa mihemko na kushabikishwa ama hasira, linapofikia swala la maamuzi ni jukumu la kila mmoja kujua, kutii na kufuata sheria ambazo tumejiwekea wenyewe kama
taasisi.

Ndg zangu wanec, wengi wenu mpo katika kugombea ubunge, udiwani, ubunge wa afrika mashariki, uwenyekiti wa halmashauri, umeya na kadhal

kadhalika, msijaribu kushiriki jaribio ambalo mnaliona dhahiri kwamba halitafanikiwa, mtajipoteza wenyewe maana mnashindana na taasisi ambayo ndio dhahiri itasimamia na kupitisha majina yenu ili mkapate dhamana mnazoomba. Kumbukeni kwamba, chama ni kikubwa kuliko mtu.

Kumuamini mgombea wako ni jambo moja, na nidhamu katika chama ni jambo lingine, na maamuzi ya vikao ambavyo kila ngazi imepewa utaratibu wake wa kikanuni ni jambo lingine pia, utii na nidhamu ya kichama ni jambo lingine.

Zingatieni.

Kupigia kura watu mahiri watatu kati ya watano mnaoletewa bila ya rushwa, urafiki, undugu n.k , bali kwa kubeba dhamana ya kuisaidia nchi kupata kiongozi bora atakayewavusha watanzania.

Kumbukeni,
Kuna msemo wa wahenga usemao "mkumbo unaua"
Lakini pia upo usemi maarufu usemao "ya rabi nafsi yangu"
Na pia upo msemo usemao "asiyesikia la mkuu uvunjika guu"

Mwenye sikio, basi ni heri kwake asikie.
 
Hao wamenunuliwa kwa nini mjumbe wa NEC ambaye ni mpiga kura uonyeshe wazi kumuunga mkono mmoja wa wagombea, pia hii ni aibu kubwa kwa Wenyeviti na Wabunge waliojipendekeza kwa mgombea aibu aibu....
 
Hii mbona kama blackmail. Kwamba wakumbuke vile walivyonavyo na jinsi watavyovipoteza kama tu watafanya yale yasiyopendwa na wewe mtoa ushauri. Nadhani wao ni watu wazima, mpaka kufikia kufanya hivyo watakuwa wamepima yote yaliyo katika nafasi ya kupotezwa na kufanya maamuzi sahihi kutokana na utashi wao wa kijamii na hata kisiasa. Nadhani ni vyema nawe kutafakari ushauri wako katika nafasi yako.

Asante
 
Back
Top Bottom