Ushauri kwa wahitimu wa vyuo vikuu

Ushauri kwa wahitimu wa vyuo vikuu

socket

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
305
Reaction score
435
Kwanza kabisa nawapongeza wahitimu wa vyuo vikuu kwa kumaliza moja ya hatua za muhimu katika safari ya mafanikio, just imagine you have stay at class for 16yrz, 17yrz na wenzetu Madaktari ni 18yrz na sasa mmemaliza na kupata vyeti. Lile chujio la kuanzia darasa la saba mwisho mmebaki ninyi.
Ushauri kwa wale wasiojua pa kuanzia, kwangu mm naweza kuwashauri mambo mawili
Kwa wale wenye uwezo kiuchumi na wanaopenda kujenga uzoefu na kuwa na xperience mapema basi nawashauri kujitolea katika mashirika binafsi for FREE yaaan bure, yaaan unatarget mahali ambapo unajua ukikaa kwa mwaka au miezi 6 basi we we utakuwa sio katika rank nyingine ya juu. Hapa cha kufanya ni kuandika CV na cover letter uwe na lengo moja tuu la kujitolea na sio kuomba 1 kazi na habari ya malipo yawe maamuzi yao na wakikubali usifanye mistake katika juhudi ya kazi
- faida ya kujitolea mbali na kuwa na experience Basi utakutana na watu mbalimbali kutoka company mbalimbali na utakuwa na wigo mpana wa kupata kazi.
Njia ya pili kwa wale wenye uwezo wa chini na pengine na familia inakutegemea basi cha kufanya ni kuwa na mtaji mdogo uko mjini basi angalia vijiji vinavyokuzunguka then fanya biashara kulingana na uhitaji wa pande mbili, mfano unaweza kutoa mayai kijijini na kuleta mjini kwa faida ya wastani na kutoa sukari mjini kupeleka kijijini, hii
Faida yake Itakusaidia kujenga foundation nzuri kiuchumi na kunguza stress za maisha kwa asilimia kadhaa.
Karibuni na wengine kuwashauri vij@na Wenzetu njia tulizotumia kujikwamua kiuchumi, mm nilijitolea for free ila baada ya mwezi ilinilipa sana.
 
...
Ushauri kwa wale wasiojua pa kuanzia, kwangu mm naweza kuwashauri mambo mawili
Kwa wale wenye uwezo kiuchumi na wanaopenda kujenga uzoefu na kuwa na xperience mapema basi nawashauri kujitolea katika mashirika binafsi for FREE yaaan bure, yaaan unatarget mahali ambapo unajua ukikaa kwa mwaka au miezi 6 basi we we utakuwa sio katika rank nyingine ya juu. Hapa cha kufanya ni kuandika CV na cover letter uwe na lengo moja tuu la kujitolea na sio kuomba 1 kazi na habari ya malipo yawe maamuzi yao na wakikubali usifanye mistake katika juhudi ya kazi
- faida ya kujitolea mbali na kuwa na experience Basi utakutana na watu mbalimbali kutoka company mbalimbali na utakuwa na wigo mpana wa kupata kazi.
...
Binafsi huo ni ushauri ninaoutoa kwa vijana wanaosoma elimu ya juu au waliohitimu. Aghalabu, huwashauri wanunue na kusoma kitabu cha Mastery, cha Robert Greene. Chambuzi zake ziko hapa. Kitabu hicho kinasema kwa urefu yale uliyoyashauri kwenye posti yako.

Kadhalika, wahitimu wengi inabidi warekebishe matarajio yao ya stahiki za ajira ya kwanza, wanazodhani watazipata kwa vile tu wana vyeti vya kuhitimu.

Halafu wahitimu hao wengi wanahitaji kuwa wanyumbufu ili wazione na kutumia fursa
 
Nakumbuka wakati nimemaliza chuo nilijitolea organizatio flani hiv BUUUUUREEEE kabisaa silipwi hata 10 kwa 5months lakini unafanya kazi, ikija suala la pesa unaambiwa unajitolea watajibu nini wakija WAKAGUZI, ikatokea wanatafuta watu kama mimi ila wakujitolea nikawaambia jamaa zangu tuilomaliza nao wanazunguka DSM hwataki kuachia JIJI na kusema tutafanyaje kazi bure

Mwezi mmoja baadae nilikuja kupewa mkataba with full package life likaanza kusonga, Mungu si athumani nilikuja kukutana na watu mbalimbali wakanielewa sana kazi wananileta binafsi nafanya daahh sikuamini asee,

PATIENT PAYS
 
Back
Top Bottom