Rohombaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 13,065
- 10,384
Mbwa ni mnyama anayependa kula sana, kila akionacho kilichonona au chenye harufu nzuri basi hukitamani na hili hasa huwapa shida sana wafugaji wengi.
Dawa ya kulidhibiti hili ni kumlisha chakula bora mara kwa mara ili awe ameshiba wakati wote na siyo kumfunga mnyororo shingoni kwani akipata nafasi kidogo tu hutafuna chochote kilicho mbele yake bila kujali kama ni chakula kweli au sumu.
Tatizo kubwa la wafugaji wengi kama siyo wote ni kutokuwa na uwezo wa kumfanya huyu mbwa ashibe. Wafugaji wengi hukosa kipato hadi siku 5 kila mwezi na wakati huu wengine huwa hawana habari kabisa na mbwa kwani huwaacha wakizurura hovyo mitaani na hii ni hatari kwao pia kwani huyu mbwa anaweza kula kunguru huko mitaani akaleta sumu hadi kwa mfugaji wake. Wale wafugaji walio makini katika kipindi hiki bado hukaa na mbwa wao na huweza hata kuwapa makaratasi kwa picha ya samaki na mbwa wao wakashiba wakaridhika.
Changamoto kuu ni pale wafugaji wanapoannza likizo bila malipo ya wiki kama 40 hivi, hapa ndipo mbwa koko wengi hutengenezwa. Hata kama mbwa alikuwa mzuri vipi lakini kama kila akiwepo nyumbani chakula hakuna na mbaya zaidi wengine hufukuzwa kwa kupigwa mawe hivyo huishia kula jalalani hivyo huweza kusababisha hatari kwa mbwa na mfugaji wake.
Kwa wafugaji waliomakini kipindi hiki hukaa na mbwa wake kwa mapenzi makubwa huku akiendelea kumpa hata supu ya magazeti na picha za nyama choma ( oro au BJ)ili mradi asiwe na njaa kali wakati wa kipindi hiki kigumu.
Mbwa akiisha geuga mbwa koko ni vigumu sana kumrudisha. Mbaya zaidi akiwa na njaa kali na wewe umemfunga mnyororo huweza hata kuwajeruhi wadada wa nyumbani au hata wadogo zako.
Ushauri: Dawa ya kumdhibiti mbwa ni shibe, shibe ya aina yoyote iwe ya kweli au feki. Mshibishe mbwa akufurahishe mfugaji
Source: Nilimsikia bibi mmoja huko inakotoka gesi huko bondeni