Naomba nianze kwa kusema hakuna aliyemkamilifu chini ya jua na siku zote mtu mwenye hekima anapotambua mwenyewe kuwa amekosea au kuonyeshwa na mtu mwingine kosa hujirekebisha na kisha kusonga mbele. Wabunge wangu wa CHADEMA inaonekana ninyi ndio hamtumii vizuri kanuni za Bunge.Tunafahamu kuna propaganda za wabunge wa CCM zinazorushwa kwenu na saa nyingine lugha za maudhi lakini mimi binafsi nawaomba na kuwashauri mtumie vizuri kanuni za bunge na mahali inastahili kutumika mnapotaka kujibu hoja za wenzenu wa CCM.Kwa mfano ktk kikao cha leo Mbunge wa Iringa mjini alionekana kutumia kanuni isivyo alipokuwa akitoa taarifa yake (badala ya kutumia kanuni ya kutoa taarifa alitoa kanuni ya kuomba mwongozo).Tunaomba msifanye vitu ambavyo vitawaondolea heshima yenu kwa wananchi ambao wanawaamini. Pia nafahamu mna kuna mambo ya kuwaudhi humo bungeni wakati vikao vinapokuwa vinaendelea kama kejeli na mambo mengine mengi na saa hamuwezi kukaa kimya na ni vizuri kuwajibu, binafsi nawashauri mjikite kwenye mambo ya kuwatetea wananchi na mambo yanayoleta maendeleo kwa taifa letu. Mwisho nawatakia kazi njema mnayoifanya hapo bungeni.