Ushauri kwa wabunge wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa wabunge wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PAMBANA, Jul 3, 2012.

 1. P

  PAMBANA Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba nianze kwa kusema hakuna aliyemkamilifu chini ya jua na siku zote mtu mwenye hekima anapotambua mwenyewe kuwa amekosea au kuonyeshwa na mtu mwingine kosa hujirekebisha na kisha kusonga mbele. Wabunge wangu wa CHADEMA inaonekana ninyi ndio hamtumii vizuri kanuni za Bunge.Tunafahamu kuna propaganda za wabunge wa CCM zinazorushwa kwenu na saa nyingine lugha za maudhi lakini mimi binafsi nawaomba na kuwashauri mtumie vizuri kanuni za bunge na mahali inastahili kutumika mnapotaka kujibu hoja za wenzenu wa CCM.Kwa mfano ktk kikao cha leo Mbunge wa Iringa mjini alionekana kutumia kanuni isivyo alipokuwa akitoa taarifa yake (badala ya kutumia kanuni ya kutoa taarifa alitoa kanuni ya kuomba mwongozo).Tunaomba msifanye vitu ambavyo vitawaondolea heshima yenu kwa wananchi ambao wanawaamini. Pia nafahamu mna kuna mambo ya kuwaudhi humo bungeni wakati vikao vinapokuwa vinaendelea kama kejeli na mambo mengine mengi na saa hamuwezi kukaa kimya na ni vizuri kuwajibu, binafsi nawashauri mjikite kwenye mambo ya kuwatetea wananchi na mambo yanayoleta maendeleo kwa taifa letu. Mwisho nawatakia kazi njema mnayoifanya hapo bungeni.
   
 2. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  TUMEPOKEA USHAURI WAKO,HATA SISI UNATUGUSA SANA,TUNAUPITIA TUTAUFANYIA UPEMBUZI YAKINIFU IKIBIDI TUTAUNDA TUME KUUCHUNGUZA HALAFU LIWALO NA LIWE LAZIMA MWISHO WA SIKU UDHAIFU UTACHUKUa MKONDO WAKE
   
 3. 2

  2015 Senior Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ukiomba mwongozo haupewi nafasi, ukisema huu sio utaratibu hausikilizi wala kupewa nafasi, inabidi mbunge wa chadema ajifanye ana taarifa kumbe ni mwongozo au huu sio utaratibu ili mradi tu apate nafasi, kwa taarifa yako wabunge wa chadema wanalazimika kutumia kanuni zisizo ilimraadi wapate nafasi, ccm hata wakikohoa tu makinda anaitikia akidhani wameomba mwongozo. dawa ya moto ni moto, wabunge wangu endeleeni kutumia kila njia kuwanyosha hawa magamba
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Sikutegemea kama lengo lango ni kutoa ushauri wa matumizi ya kanuni ndugu yangu, hawa wabunge wa CHADEMA wanasimamia mambo makubwa sana kwa niaba ya watanzania, wanasimamia maslahi ya watu wa Mwanza,Mara,Kagera,Kigoma,Shinyanga.Tabora,Singida,Geita,Simiyu,Arusha,Kilimanjaro, Dalesalama, Tanga.Lindi,Mtwara.Iringa,Mbeya.Songea,Unguja na Pemba.

  wanafanya hivyo huku wakitambua kwamba maeneo hayo mengine yanawawakilishi waliochaguliwa na wananchi kuwapigania kutoka vyama vingine, ni bahati mbaya sana kwamba wamefika bungeni na kuanza biashara zingine, katika mazingira kama haya bado unataka kuifanya issue ya kukosea kanuni kuwa issue kweli kweli?
   
 5. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa Chadema pia ni binadamu, wanakutana na maudhi mengi sana, na wanafanywa kama watoto wa kambo... nawasifu sana kwa kuweza kuvumilia upuuzi wa hali ya juu ambao kwa utu wa kawaida hauvumiliki. nwakubali sana hawa makanda!
   
 6. K

  KISWAHILI Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Simbachawene amepona mkono alioumia kule Singida?viongozi wa Mjengoni(wanaoliendesha) ni Dhaifu
   
 7. P

  PAMBANA Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na micho mnayotoa na nilikuwa sifahamu kama saa nyingine inawalazimu kufanya hivyo maana wanapoomba miongozo, utaratibu na taarifa hawapewi nafasi.
   
 8. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kwa hali iliyosasa hata Spika anasema anatumia kanuni za Bunge Lakini ukweli ni huu kuwa hata mtu yeyote anajua kuwa kuna upedeleo wa wazi kuhusu utendaji wa spika na Wenyeviti wake.
  Mbunge wa Sikonge alisema kuwa " mwenye uchungu akazae" aliyasema haya huku akichangia bajeti kila mytu anajua mbunge huyu hakuwa anachangia suala la Afya lakini Naibu Spika akasema si tusi wala si kosa.
  Jana Mwenyekiti anapombwa mwongozo kwa kanuni yeye anatoa mwongozo kuwa Tundu Lisu anataka umaarufu
  Baadaye anamtukana Mnyika kuwa "anawashwa" huyu ni mtu anayeonekana kuwa mzee wa kuaminika ndani ya CCM na kwa taifa anatumia misemo ya mateja mitaani.
  Wabunge wetu endeleeni kusimamia hoja mjikaze ili kuepusha hasira katika haya mazingira WANANCHI TUNAONA,TUNASIKIA,TUNAJUA na sasa tumeshatoa hukumu ambayo munaiona katika mikutano yenu kwa imani inayooneshwa na WANANCHI juu yenu.
   
 9. P

  Prezda wa vijana New Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwakumbusha wabunge wengi wa CDM ni wanasheria hvyo wanajua wanachofanya
   
 10. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Ujumbe umefika najua wabunge wetu wataufanyia kazi kwani ni waelewa sana na ni watu makini!
   
 11. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wabunge wa CDM pamoja na uchache wao wanastahili pongezi kwa kuwawakilisha wananchi wa Tanzania nzima. Kwani wabunge wa magamba wanakiwakilisha chama chao tu na wamewatelekeza wananchi waliowachagua na kuwatuma bungeni.
   
 12. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mkuu,lakini tambua kuwa kanuni zinakuwa zinaheshimika pale znapotumika ipasavyo bila kumkandamiza mtu!
   
 13. m

  mr arsenal Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hakika yule mwenyekiti wa kikao cha jana jioni hasitahili hata kuongoza familia yake binafsi licha ya kupewa nafsasi ya kuonekana mjengoni.
  Baada ya kuharibu mwishoni anajikosha o- wabunge naomba tutumie kanuni. Shame on you gamba!!!
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wabunge wote should grow up and discuss issues kama watu wazima, do you realise even your own kids and grand kids watch you guys shouting at each other on the telly...its disgusting to say the least
   
 15. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  nakuunga mkono mkuu ,upo sahihi
   
Loading...