Ushauri kwa vijana mnaopenda siasa za vyama

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,401
USHAURI KWA VIJANA MNAOPENDA SIASA ZA VYAMA.

''Vijana wenzangu wapenda Amani tu, ukiona mwanaharakati anapigania Amani huyo ni bora na yuko salama lakini ukiona mwanaharakati anapigania Siasa ya vyama huyo yuko hatarini.

Amani ni juenzi wa jamii mpya katika kuleta fikira mpya ya kujenga Tanzania mpya.'' by Kisandu

Mimi ni Mwana CCM naipenda siasa lakini siwapendi Wanasiasa na ndio maana na Napenda amani siku zote katika nchi yangu, naipenda CCM yetu kama navyojipenda mwenyewe. Sipendi siasa za majungu, fitina na kejeli na upotoshwaji wa uhalisia wa mambo mema kwa Taifa.

Siku zote ni heri Amani moyoni kuliko vurugu Rohoni. Ukitaka kuwa Mwanasiasa mzuri penda zaidi siasa za kujenga Nchi na kuunganisha Watanzania na utakuwa na Amani moyoni hata kama utawekwa vizuizini maana wanajua fika wewe ni HADHINA YA TAIFA. Lakini ukitaka kuwa Mwanasiasa bambucha utajikuta siasa zako zimejaa Personal Attacks na sio kusahihisha. Mwanaharakati mzuri ni yule anayekosoa na kutoa suluhisho la ukosoaji wake. Yesu alikuwa akiwakosoa maadui zake na kuwapa suluhisho la nini wafanye ili wawe wema.

Ukiwagawa watu lazima wakugawe na wewe lakini ukiwajenga watu lazima nao Mungu atawagusa nao watakujenga kwa kukupa Tuzo ya Heshima. Wanaharakati wote Duniani kama kina Malcom x, Bicco, Mandela, Nyerere, Nkruma, Obama, kenedy, Tuntemeke Sanga na wengine wengi walikuwa wanafanya harakati za siasa za Usuluhishi ili kudai mahitaji ya watu wao kwa kutumia hoja suluhishi na sio hoja chonganishi na ndio maana wapo walio wekwa vizuizini na wengine kupewa Tuzo ya kuongoza nchi kulingana na hoja zao zilivyosaidia nchi zao.

Huwezi ukapewa nchi kama unauponda utawala uliopo ila utapewa nchi kama unaujenga utawala uliopo. Mtangulizi wako hata kama anamapungufu unatakiwa kumrekebisha ili ajisahihishe pale alipokosea nasi kumkashifu, rejeeni kitabu changu ''UTANI WA SERIKALI NA WANANCHI'' ambacho kila Hoja niliyoikosoa nchi yangu mwishoni nilitoa Suluhisho ili kujenga nchi upya yaani tiba mbadala.

Siasa sio kusaka pesa wala kutafuta jina kubwa bali siasa ni kujengana kifikira bila kumdhalilisha mwingine.
Wadogo zangu kwa umri wangu wa miaka 35, mimi Deogratius kisandu nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Dunia nzima tangu nikiwa mtoto kwa msaada wa marehemu mzee wangu na wadau mbalimbali wakiwemo Madre na Masheikh walioanza kunijenga tangu mtoto. Nawasihi msifanye siasa za mihemko na mikumbo kwa maslahi ya Taifa letu.

Brother Kisandu.
Mtumishi Mdogo sana wa Mungu.
15 Nov.2015
 
Haya mwana ccm ...lumumba wamekusikia kachukue chako....
 
Umezunguka vyama weee..mwisho umetupwa kwenye dust bin .. Amani ni zao la haki... Kitendo cha ccm kuiba kura za Lowasa na Kumnyima Maalim Seif urais kilichofanywa na ccm ni cha kidhalim sana
 
Anayevuruga amani ni ccm na ndio anataka wazanzibari waingie mitaani ili wawaue
 
Umeongea vyema mkuu na wenye chembe chembe za kusiki? watakuelewa vizuri sana
 
$$$$$$iiiit.
 
Kisandu....

from CDM to NCCR to CCM....

Kwako siasa ni zaidi ya chama
..
 
Anayevuruga amani ni ccm na ndio anataka wazanzibari waingie mitaani ili wawaue

Ndo mwisho wa mawazo yako wamevuruga amani wapi kuna mtu anakuuliza maswali juu ya unavyoishi au familia yako acha ushabiki mkuu usio na tija mkuu
 
Umezunguka vyama weee..mwisho umetupwa kwenye dust bin .. Amani ni zao la haki... Kitendo cha ccm kuiba kura za Lowasa na Kumnyima Maalim Seif urais kilichofanywa na ccm ni cha kidhalim sana

mbona hamjaibiwa arusha au Kilimanjaro!? mkishinda nyinyi ni sahihi mkishindwa mmeibiwa!
mawazo kama hayo ni nyumbu tu anayoweza kuwa nayo siyo binadam
 
Umezunguka vyama weee..mwisho umetupwa kwenye dust bin .. Amani ni zao la haki... Kitendo cha ccm kuiba kura za Lowasa na Kumnyima Maalim Seif urais kilichofanywa na ccm ni cha kidhalim sana
Naakili zako LOWASA nani kamuibia kura! hebu amkeni pale mlikuwa na MDOLI SI MGOMBEA mlitaka tupeleke nini IKULU!
 
Back
Top Bottom