Ushauri kwa uongozi mpya wa ccm

Nyami2010

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
227
50
Kwa uongozi mpya wa CCM ninaomba ninawapeni ushauri wa bure kama ifuatavyo:

1. Hakikisha MAFISADI WOTE wanatoswa na kamwe wasirudi kundini;

2. Fanya mabadiriko kwenye katiba yenu, imepitwa na wakati;

3. Fanyeni mageuzi kwa kuwapatia vijana nafasi za uongozi ndani ya chama kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata, wilaya, mkoa na taifa;

4. Uongozi mpya uwatafute wale wote waliotoswa kwenye kura za maoni katika chaguzi za CCM - 2010, wawasiliane/wakutane kwa mikakati na majadiliano zaidi;

5. Mwenyekiti Taifa na kama Mkuu wa Kaya, ahakikishe wale wote waliotoswa kwenye chaguzi za kura za maoni, wanarudishwa kundini kama watetezi Imara wa Chama

6. Katika chaguzi za mbeleni, ombeni msaada wa utaalamu kutoka Tume ya Uchaguzi.

Kama mkizingatia haya, sina shaka kuwa CCM itaendelea kuwa Imara Tanzania.

NB: Sina uanachama na chama chochote cha siasa. Ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom