Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Baada ya serikali kusitisha urushwaji wa moja kwa moja wa shughuli za vikao vya Bunge,nashauri hotuba zote za mawaziri vivuli ziwe zinasomwa katika vituo binafsi vya Television na Radio.Hotuba hizi zirekodiwe na ikiwezekana pia mawaziri hawa wazisome hotuba hizo live.
Wabunge wa UKAWA mko zaidi ya mia moja hivyo mnaweze kuchangishana ili kupata fedha za kugharamia airtime hizo na pia mnaweza kutumia ruzuku za chama kugharamia matangazo hayo.Vile vile mnaweza kuweka utaratibu na wananchi wakachangia.
Mbali na hotuba za mawaziri vivuli, hata hoja binafsi za wabunge wa UKAWA zitakazokubaliwa kuwasilishwa Bungeni zisomwe pia katika vipindi hivi mtakavyoviandaa kwa kushirikiana na vituo binafsi vya Radio na Television.
Cha msingi mlenge kurusha vipindi hivi katika muda ambao watu wengi watakuwa katika nafasi nzuri ya kufuatilia hotuba hizi kama vile mara baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku.
Hotuba hizi mnaweza pia kuzichapisha katika magazeti mbalimbali au kuandaa matoleo maalumu ya hotuba hizi na kuziweka katikakati ya magazeti yakiwemo hata magazeti ya udaku na michezo kwa makubaliano maalumu na wamiliki wa magazeti haya.
Ni ushauri tu.