Kwanza nalipongeza sana shirika hili ambalo kwa kiasi kikubwa limeweza kuonyesha kuwa watanzania tukiamua tunaweza, nimeshuhudia miradi mingi ya nyumba katika maeneo mbalimbali ya nchi hongereni sana.
Jambo ambalo ningependa kushauri shirika hili ni juu ya mikakati yao ya kujenga nyumba kwa nia ya kuuza, nafikiri ni wazo zuri ila kuna maeneo ambayo nafikiri wangejikita katika kujenga nyumba ili kuzipangisha. Kwamfano sasa hivi serikali inahamia Dodoma moja ya kilio kikubwa cha wafanyakazi wa serikali ni makazi, wafanyakazi wengi wa serikali wanaohamia Dodoma wataacha familia zao Dar es Salaam wengi wao watapenda kutafuta nyumba za kupanga ambazo zitawasaidia kuishi hapo hadi watakapo staafu au kuhamishwa, ieleweke wazi kuwa mfanyakazi wa serikali ana mwisho wa kuwepo kazini kibaya zaidi nyumba hizo kwa namna na maeneo mnapozijenga sio rahisi mnunuzi kubadilisha matumizi, kwamfano nyumba hizi za jumuia huwezi kuibadili na kuweka baa au nyumba ya kulala wageni.
Mimi nashauri kuweni na mkakati wa kujenga nyumba za kupangisha ili wale ambao hawana uwezo wa kununua nyumba waweze kupanga. Zamani wakati serikali ilipoanzisha shirika hili nafikiri msisitizo ulikuwa kujenga nyumba na kuzipangisha hili swala la kujenga nyumba za kuuzia wananchi liende sambamba na kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha maana naona wateja wake ni wa uhakika.