Ushauri kwa Serikali mkoa wa Mwanza

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,869
Reaction score
5,170
Pale kwenye picha ya samaki kile ni kivutio kikubwa kila mtu anayekuja Mwanza atataka apige picha pale.Ile bustani iko vizuri hata wapiga picha wanaitunza vizuri huruhusiwi kukanyaga majani ila pavements.Siwashitaki ila ushauri tu kwa faida ya serikali ya mkoa na sisi wananchi.

Nilitaka kupiga picha nikaambiwa nitoe mchango wa 1000 kutunza bustani.Nikawauliza nipeni risiti wakaniambia hakuna nikawauliza nitajuaje hii hela nitajuaje unampelekea mkeo?.Nikawaambia muwe na EFD mashine serikali ipate haki yake mapato mengine yatumike kutunza bustani.Nikatoka hapo nikaenda choo binafsi Kamanga shillingi 300 tu lakini nikapewa risiti toka EFD.

Naomba mkuu wa mkoa mhe peleka EFD kwa wale vijana wetu wanajitahidi kutunza mazingira ya pale ila hiyo 1000 itolewe kihalali
 
Ushauri mgine ni wakitoto sana......sasa pale 1000 kweli yanini? Picha na bustani vyenyewe haviko katika viwango vya kimataifa....sema wanao piga picha pale wengi ni wakutoka vijijini hasa wahaya na wakerewe wengi nimara yao ya kwanza kufika mwz wanaibiwa tu kwa ushamba wao. Kazi ya almashauri ya jiji nikutunza sehemu kama hizo.
 
Kuna siku nimepeleka wajukuu zangu baada ya kuhitimu darasa la saba na kufaulu vizuri nikawatoa out wakafurahie maisha nikawapitisha pale wapige picha mshenzi mmoja akataka kuwazuia walipie nikashuka kwenye ngalala yangu ya mjapan nikamwambia kijana kama una hati milki ya hii garden nionyeshe na hao watoto hawatapiga picha ila kama ni ni ya jiji naomba usiwabughudhi hao watoto nikakuharibia siku yako watu tupo mjini zaidi ya miaka 40 unaleta ujuaji from kaishozi
 
Kwani huyu aliekua anakupiga mkwara alikua mhaya?
 
Kwani huyu aliekua anakupiga mkwara alikua mhaya?
Kwani hujui wengi wao pale ni from kaishozi ukerewe na musoma wakishafika mjini wanataka kujifanya wajuaji kuliko hata wenye mkoa wao sasa walinikuta nami nilishapinda miaka dahari hapa mjini
 
Nimetoa ushauri kama mzalendo wa nchi yangu
 
Wewe ni Mhaya Mkuu?
 
Nani
Umeongea nini sasa, mbona sikuelewi ndio ushauri kwa serikali yako, kazi tunayo na hawa wahaya, ndio mabadiliko kwa hawa pembe ya ng'ombe sijui labda kiama
Nanimhaya mbona unalazimisha kunibatiza kabila siyo langu kulikoni?kijana
 
Nani
Mkimbizi miaka 50 niko hapa nchini jumlisha 8 ambayo nimetoka nayo Zaire nilishakuwa mtanzania kamili
Da, ongela mtanzania mwenzangu, vipi ushauri wako kuhusu vivuko vyetu mana kazi tunayo kama watanzania kukwepa, hali hii
 
Da, ongela mtanzania mwenzangu, vipi ushauri wako kuhusu vivuko vyetu mana kazi tunayo kama watanzania kukwepa, hali hii
Mkuu hili tatizo la vivuko ni viongozi na wasomi wetu uchwara na kufanya kazi kwa mazoea mtu akifanya vizuri anapigiwa zengwe mpaka anatoka ili wafanye yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…