Ushauri kwa RC wa Iringa, Ally HapI ili uiletee Iringa maendeleo

Ushauri kwa RC wa Iringa, Ally HapI ili uiletee Iringa maendeleo

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
601
Reaction score
2,508
"IRINGA MPYA" HAILETWI KWA GARI KAMA ZAWADI KWENYE BOX

Na Livino Haule & Emmanuel Chengula

Rais wa zamani wa Ghana, #KWAME_NKRUMAH* katika kitabu chake #AFRICA_MUST_UNITE kilichochapishwa na FREDERICK A. PAEGER (New York, 1963) kwenye ukurasa wa 54-55 amesema mambo ya kuzingatia wakati wa kujenga jamii huru ya Afrika kuelekea maendeleo;

1. Go to people
2. Live among them
3. Learn from them
4. Love them
5. Serve them
6. Plan with them
7. Start with what they know
8. Build on what they have.

Kwa Kiswahili Nkrumah anatushauri kama ifuatavyo;
1. Nenda kwa watu
2. Ukaishi miongoni mwao
3. Ukajifunze kutoka kwao
4. Kuwa hakuna lolote au hakuna walichokifanya cha maana.
5. Ukawatumikie
6. Ukapange pamoja nao
7. Ukaanze na kile wanachojua wao
8. Ukajenge/Ukaendeleze kile walichonacho wao.

Hizi ni "guides" ambazo Nkrumah alizitumia kuwaelekeza watu waliokuwa wafuasi/wanachama wa chama chake kipya cha C.P.P (Convention People's Party) baada ya kujiondoa kwenye chama cha awali cha U.G.C.C (United Gold Coast Convention) tarehe 12/09/1949.

RC anashauriwa kuzingatia miongozo hiyo kama kweli anayo nia ya kusaidia Serikali za Mitaa (Halmashauri) zilizopo ndani ya maeneo ya utawala wao, kama anavyoamriwa na _Sheria ya Tawala za Mikoa (Regional Administration Act) CAP 97 R.E 2002; chini ya KIFUNGU CHA 5 (2) (3)_ kikisomwa pamoja na Sheria zingine 13 zilizoprodheshwa katika _NYONGEZA YA KWANZA (First Schedule)_ ya Sheria hiyo.

RC analetwa kuanza kazi Mkoa wa Iringa hatakiwi kufika tu na kudhania kwamba watu anaowakuta pale "hawana lolote" ila yeye ndiye anawaletea maendeleo sasa, jambo ambalo sio sahihi hata kidogo.

Ni lazima atulie huku akijifunza na kutathimini ni maeneo gani RCs waliopita na viongozi aliowakuta wamefanikiwa, na sehemu gani bado hawakufanikiwa; na kitu gani kinahitajika zaidi.

*IRINGA MPYA* _haiwezi kuletwa kwenye Box kama zawadi kutoka Kinondoni ambayo RC anaweza kudhaniwa kuibeba_

BALI Iringa Mpya ni "muunganiko" wa mawazo na fikra chanya zilizojengwa katika muundo wa ushirikishwaji kuanzia:

(a) WANANCHI (wakazi wa iringa),

(b) WAWAKILISHI WAO (Madiwani wa iringa),

(c) WATUMISHI WA UMMA (Watumishi/wafanyakazi wa taasisi za serikali),

(d) WATENDAJI WA SERIKALI (Wakurugenzi, maDC, na wakuu wa Idara mbalimbali), pamoja na;

(e) VYOMBO VYA DOLA (Taasisi za Ulinzi na Usalama) zilizopo katika mkoa huo.

Wazo lolote jipya ambalo RC amekuja nalo ambalo anahisi litafaa kufanyiwa kazi ili kufanikisha malengo ya kimaendeleo mkoani humo, sharti lipitie kwenye NGAZI YA USHAURI (Regional Consultative Committee) iliyoundwa kwa mujibu wa _Kifungu cha 8 cha Sheria ya Tawala za Mikoa_ ili wazo hilo lipimwe na kuzingatiwa na Kamati hiyo kwa kuzingatia Kifungu cha 9 cha Sheria hiyo.

Huwezi kuwahesabu Madiwani uliowakuta, RC aliyestaafu, DCs uliowakuta, Wakurugenzi waliopo, Watendaji wote, Afisa Tarafa uliowakuta, Mbunge wa Wananchi aliyepo, Wauguzi na Madaktari, maafisa ustwi wa jamii, maafisa maendeleo, Walimu waliopo, Askari uliowakuta, Watendaji wa Mamlaka ya Maji (IRUWASSA), Watendaji wa TANESCO, Wasimamizi wa Soko, Watendaji wa TARURA,etc. kama hawajafanya la maana na hawana walijualo isipokuwa wewe RC mgeni ndio mkombozi uliyesubiriwa. That's is Illusion/ fallacy.

Kiongozi mzuri angeuliza waliopo;

○Wana mipango gani ya maendeleo,
○Wameanza wapi/wameanza na nini,
○Wamefikia hatua gani,
○Wanakabiliana na changamoto gani,
○ Wapi wamefeli kabisa,
○Wangependa yeye RC asaidie sehemu gani kwa nafasi yake.

KWA KUWA RC ni daraja kati ya Serikali za Mitaa (Local Governments/Halmashauri) na Serikali Kuu/Rais wa nchi, kama ilivyoainishwa katika *IBARA YA 61 (1) Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, 1977;* basi wajibu wake baada ya kupata majibu ya maswali hayo ni kufikisha kwa ukaribu zaidi maombi ya Halmashauri hizo kwa Serikali Kuu/ kwa Rais wa nchi ili kupata suluhu yakinifu au Yale yaliyopo kwenye uwezo wake akayatatua kwa kushirikiana na wakuu wa idara kuliko kuwashughulikia watumishi kama vile wapo mahakamani , eti inaitwa mahakama ya wazi, real? Iringa mpya haijengwi kwa kuhoji watumishi hadharani tukidhani watakumbuka file zote zilizopo ofsini kwao, watanzania hatujawa na akili hii.

Hii ni kwa sababu RC ni MLEZI wa Serikali za Mitaa zilizopo katika mkoa wake.

Huu ndio wajibu wake wa msingi; _kumsaidia Rais/Serikali Kuu kuhuwisha na kuzilea Halmashauri hizo na kuzisaidia kutekeleza Mipango na Sera za serikali, pamoja na kusimamia Sheria za Nchi (Law enforcement) ndani ya mkoa wake,_ kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Tawala za Mikoa.

Pia RC wajibu wake ni kuzisaidia Halmashauri zake kutekeleza _Wajibu na Majukumu yake_ yaliyowekwa kisheria kwa mujibu wa Vifungu vya 113 na 114 cha Sheria vya Serikali za Mitaa/The Local Governments (District Authorities ) Act, CAP 287 R.E 2002

○Ili kupata jamii yenye Utaratibu, Amani na Utawala bora.

○Ili kujenga na kuimarisha Mkoa wenye Raia wenye Uchumi imara na Ustawi wa jamii yao.

○Ili kufanya mazingira bora ya kutekeleza Sera na Mipango ya Taifa ili kuleta maendeleo katika Vijiji na Miji iliyopo mkoani kwake.

○Kuwezesha Mkoa wake kujipatia jamii zenye Ushirikishwaji wa Kidemokrasia.

○Kuziwezesha Halmashauri za Mkoa wake kubuni na kusimamia Vyanzo imara na endelevu vya Mapato yake kwa maendeleo yake na Taifa kwa ujumla. N.k.

RC anao Wajibu chini ya KIFUNGU CHA 5 cha sheria ya Tawala za Mikoa, Kuwezesha Halmashauri zake kutekeleza majukumu yote yaliyoorodheshwa katika NYONGEZA YA KWANZA NA PILI (1st & 2nd Schedules) za Local Government ( District Authorities) Act, zitokanazo na Vifungu vya 122 (4) na 144 (1) vya sheria hiyo; ikisomwa pamoja na Kifungu cha 60 & 66 cha The Local Government ( Urban Authorities) Act, CAP 288 R.E 2002.

Inakuwaje RC kama Mlezi wa Serikali hizo za Mitaa anakuja kuvuruga, kugombana, kudhalilisha na kukejeli viongozi na Watumishi wenzake wanaofanya kazi katika taasisi mbalimbali? Je matendo hayo yanawajengea kujiamini watumishi au hofu na woga kwa wanaowatumikia?

Je, Iringa Mpya itapatikana kwa kuwaweka Mahabusu Madaktari na Wauguzi, wahandisi wa umeme, Maafisa wa Halmashauri na Madiwani wa kata mbalimbali?

Je, kwa kufanya hivyo; ndio maana ya kuzisaidia Halmashauri hizo au kudidimiza morali/Ari ya kufanya kazi kwa watumishi wa umma?

Au Iringa Mpya itapatikana kwa kuwakataa baadhi ya Watumishi wa Umma wasionekane kwenye mkoa wetu? Hii ndo iringa mpya? Not at all.

Tatizo kubwa ni kwamba maRC wetu wengi hawasomi kujua kwa dhati sheria inayowaongoza inawapa Haki, Wajibu na Mamlaka gani. Au hawawatumii washauri wao wa sheria ili kufahamishwa the DOS na DONTS.

RCs wetu wanachokijua wao ni Mamlaka ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Tawala za mikoa ya 1997 kwa kuagiza mtu yeyote kuwekwa Mahabusu masaa 48, ila hawajui "conditions" na "Compliance requirements" zilizowekwa katika Kifungu hicho.

MaRC wetu wajifunze kutafiti/kusoma au kuuliza kwa wanaojua mambo ili kujiridhisha kabla ya kuchukua maamuzi yoyote.

RC unashauriwa kujifunza na kuzingatia GUIDELINES 8 alizosema *KWAME NKRUMAH,* kwahizo utapata heshima njema zaidi kuliko kutafuta Umaarufu kwa kuvunja sheria na kuumiza watu wasio na hatia.
 
Yule ni kada,na kaenda pale kwa kazi maalumu/kimkakati wa kurejesha jimbo kutoka kwa 'magaidi'... Ni mwendo wa kick tu mpaka muuelewe u-hatari wake na hachezewi.. Kazi nzuri na ya kutukuka atakayofanya ni kumuondoa Msigwa pale mjini... Hayo mengine fanyeni wenyewe.
 
Thanx mkuu Goliath Mfalimagoha & job done!...thats a "nail on the neck"
 
Back
Top Bottom