Ushauri kwa rais kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa rais kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by peoplespower54, May 2, 2012.

 1. p

  peoplespower54 Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni Mtazania na naipenda sana nchi yangu. Nasikitishwa sana na utendaji mbaya wa viongozi na watawala wa nchi hii. Leo nitazungumzia nafasi ya Rais na Watendaji wake katika ngazi mbalimbali.

  Nimekuwa nikisoma sana makala, story na tips mbalimbali ambazo zinamkashfu Rais. I will be very objective on this. Kwa upande mmoja ni kweli lazima Rais alaumiwe kama msimamizi wa rasilimali za nchi hii lakini kwa upande wa pili namsikitikia sana Rais kwa sababu aliowaamini wanaweza kumsaidia wanafanya mambo ya kijinga sana na ndio wanamfanya Rais anaonekana hafai. Kwa lugha za mtaani vijana wanasema "yaani mshikaji wakao anakukatia pande halafu wewe unamwangusha bwana!" Hiki ndicho wanachofanya watendaji wa Rais Kikwete.

  Leo nimeamua kujitosha kuonyesha udhaifu wa serikali ya Kikwete uko wapi. Ni ukweli mtupu kwamba serikali ni mnyororo. Una watendaji ngazi zote. Hebu tuchukulie mfano huu: Rais amewateua wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimamizi wake katika halmashauri. Chini ya Mkurugenzi wako wakuu wa idara mbalimbali kama Afisa Mipango, Afisa utumishi, Mweka hazina, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari na wengineo. Kazi kubwa ya Mkurugenzi Mtendaji ni kuhakikisha wakuu wa idara wanatekeleza IPASAVYO majukumu aliyowapangia. Lakini cha kusikitisha watendaji hawa wa serikali wamekuwa tu kama "WASHIKAJI". Suala zima la KUWAJIBISHA wakuu wa idara limekuwa ngumu sana na hivyo wakurugenzi hawana meno hata kidogo kwa wakuu wa idara. Hili nalo limeathiri sana watendaji walioko chini ya wakuu wa idara. Wakuu wa idara nao wanawaonea aibu subordinates wao. Kwa hiyo uozo wa serikali umeanza chini kabisa ndio maana hata Rais hawezi kufanya chochote. Kuwaondoa mawaziri siyo hoja, hoja ni je; mfumo mzima wa uongozi unatewajibika ipasavyo?

  Kwenye halmshauri siku hizi kila mtu kijogoo. Kila mtu ana ndevu. Hili linatokana na ukweli kwamba watendaji wakuu kama Wakurugenzi wamekosa UADILIFU. Kama mkurugenzi anashirikiana na baadhi ya wakuu wa Idara kula fedha za umma, iweje ageuke tena kuwa hakimu wa anaekula nae? Kwa hiyo pamoja na udhaifu alionao Rais wa kutokuwawajibisha mawaziri na makatibu wakuu lakini watendaji wake na nafasi ya mtumishi mmoja mmoja haipo. Lawama hizi zote lazima ziende pande zote.

  Namalizia kwa kumnukuu Baba wa Taifa: INAWEZEKANA, TIMIZA WAJIBU WAKO

  Asanteni kwa kunisoma, Mungu Ibariki Tanzania!
   
Loading...