Mwambie asijelogwa kufanya kama huyo jamaa anavyotaka kwani atajuta ....
Kama anataka mtoto si amuoe kabisa?
Kimsingi watu wa namna hiyo huwa ni wa hovyo sana na mara nyingi ni watesaji,mtu gani hapajui kwa mpenzi wake?
Halafu hapa naliona tatizo lingine ambalo linawatafuna wengi sana na tatizo hilo ni kuongozwa na hisia,huyo rafikiyako anaongozwa na hisia kubeba ujauzito kwa mtu ambae hata hapajui kwake na anataka kulazimisha aone ni sawa japokuwa akili yake inamkatalia
Kwenye mambo yote hapa duniani ukitumia hisia utajikuta unaingia shimoni,mwambie atumia akili mahali ambapo inatakiwa itumike na sio kutumia hisia mahali ambapo haihitajiki,ni sawa utake kutumia mikono kutembea badala ya miguu
Aweke hisia pembeni na amkatalie huyo jamaa hilo jambo la kijuha na kama jamaa ataamua kuondoka aende ........!!