pendoharri
JF-Expert Member
- Aug 5, 2016
- 508
- 306
Rafiki yangu nimempokea miezi 4 sasa tangia amefukuzwa kwao baada ya kushika mimba. Mwenye mimba ni mwanajeshi mwanzo alikuwa anatuma matumizi kama kawaida ila mimba ilipofikisha Miezi 6 akawa hatoi tena pesa za kutumia.
Binti kuona mambo yanakuwa magumu akaenda jeshini kueleza yote na alipoulizwa mwanaume kwa njia ya cm kwani amepangiwa kazi mkoa mwingine akakubali kuwa anamjua ni hiyo mimba ni yake kweli, Wakamwambia iwapo binti ataenda mbele zaidi yeye ataaribu kazi kwani muda wake wakuoa bado.
Ikabidi baba wakijana akapigiwa SImu akamfuata jeshini rafiki yangu ila kwamasharti na kuandika maelezo kuwa chochote kikitokea jeshi litasimama upande wa binti. Tatizo limekuja hapa mwanaume anataka Binti akajifungulie kwao mbeya na muda wa kujifungua umebaki wiki 2 na anapresha yakupanda.
Mwanaume hataki kuelewa na amemwambia hatumi hata mia mpka aende ukweni.Binti amelazwa presha iko juu sana madaktar wameamua kumpasua kuokoa maisha yake na mtoto.Tumejaribu kumwambia mwanaume amekuwa mkali na tokea jana amezima simu. Tunatamani kwenda tena jeshini ili apate msada wa kulipia gharama za hospital na huduma nyingine muhimu.Baba mkwe wake anaomba sana tusirud jeshini kwan mwanae kazi atakosa ila chakuumiza baba yake hatoi msaada wowote.
Wanajamvi naombeni ushauri kwani rafiki yangu yuko taabani