Tanzania Mpya
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 252
- 145
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, naomba nikupe ushauri wangu kidogo.
Naomba uliangalie suala la usafiri ktk jiji lako la Dar es Salaam. Kwa sasa hali ilivyo ni vigumu sana kwa magrupu maalumu kupata usafiri (daladala) nyakati za asubuhi na jioni. Jamii ya wasafiri au watumiaji wa usafiri huu jijini Dar kwa kweli hawajawathamini Wazee, Akina mama, Wajawazito, watoto, na walemavu ktk kupata usafiri hasa kwa nyakati hizo.
Magrupu haya yanaweza kukaa kituoni kwa muda wa masaa hata matatu bila kupata usafiri, wakati vijana wenye nguvu na wasiojali wanakuja kituoni na kutumia nguvu na kuondoka mara moja.
Naomba ktk uongozi wako mh, ufikirie utaratibu wa kupanda magari haya kwa foleni. Yaani, aliyetangulia kufika kituoni apate usafiri mapema na sio kutegemea nguvu za mtu. Utaratibu huu utawasaidia hao niliowataja hapo juu kutohangaika na usafiri wa kwenda hospitalini, makazini, mashuleni, na majumbani na pia.
Utaratibu huu unawezekana, ni kujipanga tu na kufanya maamuzi. Tuikatae aibu hii ya kutothamini wazee, walemavu, wajawazito na watoto katika jamii yetu. Wakati umefika sasa tutende haki.
Ninaamini ushauri huu utafanyia utafiti na kuona namna bora zaidi ya kutekeleza jambo hili.
Mungu akutangulie ktk kazi zako, na akuwezeshe Mkuu.
Nakutakia kazi njema Mhe.