Ushauri kwa mifuko ya hifadhi ya jamii

OMARY2012

Senior Member
Apr 2, 2012
111
225
Napenda kuishauri mifuko ya hifadhi ya jamii kama vile LAPF, PSPF, NSSF na mingine kuwa na mtazamo chanya kwa kulenga kuwanufaisha zaidi wanachama wake kwa kutoa mikopo ya riba nafuu ya nyumba, gharama za masomo na mitaji ya biashara kuliko kuruhusu serikali na wanasiasa kujichotea fedha nyingi katika mifuko hiyo. Fedha zinazochotwa na serikali na wanasiasa hazilipiki na hivyo kupelekea kufilisika kwa mifuko hii. Serikali ihakikishe kuleta marekebisho ya sheria ya kuanzishwa kwa mifuko hii ili kuwawezesha wanachama wa mifuko hii kuwa na maamuzi juu ya fedha zake kwa kuwa wajumbe katika bodi za mifuko hii. Inasikitisha sana fedha za mifuko hii kupewa wanasiasa na serikali na kuwaacha wanachama wake katika lindi la umaskini kwa kukosa makazi bora, chakula na kushindwa kugharamia Elimu yao na ya familia zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom