Ushauri kwa Membe, Jitenge na Wanafiki

Mwamakula tu ndiye anaweza ku discuss issue ya Msiba, maana alisimamia ukweli na haki. hawa wengine ni takataka.
Mwamakula anasema walimtumia mjumbe akamwambia aache kuimba mambo ya haki vinginevyo atapotea. Mtumishi wa Mungu akasema kama kuimba Haki mnataka kuniua basi kamwambie aliyekutuma aje aniue tu.

Mwamakula ni kama Meshaki, Abedenego na Shadrack kwa Nebkadineza.
 
Jipe muda, uelewe maana ya kisasi.

Kwa ufupi ni kwamba, kwa mfano wewe ukaiba mali ya mtu, yule mtu akapata ushahidi kuwa ulimwibia, akaenda kukushtaki, nawe ukahukumiwa kwa lile kosa, hicho siyo kisasi. Umeadhibiwa kwa uovu ulioufanya.

Lakini kwa mfano wewe leo hii ukaenda ofisi ya kampuni fulani kutafuta kazi,, kwenye hiyo ofisi akawepo mwajiri ambaye kwa upendeleo tu kwa watu fulani, akakunyima ajira wakati sifa unazo. Baada ya miaka kupita, wewe ukapata kazi, na yule aliyekunyima ajra hapo kale naye akaja kumwacha mwajiri waje wa mwanzo, akaajiriwa kwenye kampuni ambayo wewe sasa upo, na wewe ukawa ndiye mkurugenzi mkuu wa kampuni. Huyo bwana akafanya kosa dogo lililostahili kupewa onyo lakini ukaamua kumfukuza kazi kwa sababu tu unakumbuka alivyokutenda hapo kale, hicho ndicho huitwa kisasi.
 
Imani yangu wewe ni mmoja kati ya hilo kundi la wanafiki, ushauri wa hovyo sana huu uzungumzao
 
Imani yangu wewe ni mmoja kati ya hilo kundi la wanafiki, ushauri wa hovyo sana huu uzungumzao
Mjinga akikuambia wewe ni mjinga wakati siyo mjinga, hutakuwa mjinga kwa sababu kuna mjinga amesema wewe ni mjinga.
 
Nabaki hapo kwenye mfano wako wa mwajiri, then inakuje kama huyo jamaa akituma watu waje kukuomba msamaha kwa kosa alilokufanyia mwanzo hadi ukaenda kutafuta kazi sehemu nyingine, na baadae kupandishwa cheo, ukiukataa msamaha wake hicho sio kisasi?
 
Mbona misamaha mingine haiwi na publicity na trending kama huu?

Huu inabidi utafautishwe na hiyo mingine ya kawaida kwa sababu kila kitu chake pia sio cha kawaida.

Je Kabla ya Musiba uliwahi ona wapi mtu akitukana, kutisha, kuchafua, kufedhehesha watu namna ile, tena hadharani, kwenye mitandao na kwingineko??

Nampongeza Bw. Membe, kwani amewakilisha wahanga wengine wengi kumshughulikia yule mhuni.
 
Mkuu Bams, Inavyoonekana wewe ni mtu mzima atleast mtu wa makamo piga ua enye miaka 40-50 una elimu ya kutosha na ni mcha mungu una familia halafu unapenda haki na unaamini kuwa jinai haiozi, hupendi unafiki,unajali watu na huwa ni mtetezi wa wanyonge n.k n.k

Kitu ambacho sijaweza kudadavua hata kwa kukisia kisia huko juu ni Una asili ya Bara gani- Asili yako? Mwafrika Muarabu, Mzungu wa Ulaya, au MwaAshia n.k uniwie radhi na naomba unisahihishe kama hayo juu sio description nzuri au ina uwalakini...ila kwa kifupi naweza kusema wewe ni Mtanzania wa Asili ya bara gani haswa sijui. Ni muhimu, ni muhimu kwa swali niliokuwa nalo na nitaweza kukuuliza tu iwapo nina jibu
 
Bams uko sahihi mkuu, maana Musiba mbali na hiyo kesi ya Membe lakini pia angekuweza kuwa na kesi ya jjnai na hata kufungwa jela - ni vile basi utawala wa sheria uliwekwa ndani ya jokofu awamu ile.
 
Kweli lazima misiba alipe bilioni 8, tuache unafiki. Member alidharilishwa mkawa mnafurahia, Leo ndio mnajua Dunia inazunguka. Yani uwafanyie wengine ubaya uwachwe kisa Dunia inazunguka?. Alipe pesa za watu huyo chawa.
Hajadhalilishwa isipokuwa mipango yake ya gizani pamoja na wote aliowataja Musiba iliwekwa hadharani. Labda kosa la Musiba ni kuiweka hadharani kinyume Cha Sheria lakini tuhuma zote zilikuwa sahihi Kwa 100%
 
Fisadi tu ilo membe
Hajadhalilishwa isipokuwa mipango yake ya gizani pamoja na wote aliowataja Musiba iliwekwa hadharani. Labda kosa la Musiba ni kuiweka hadharani kinyume Cha Sheria lakini tuhuma zote zilikuwa sahihi Kwa 100%
 
Bandiko reefu,kiko wapi sasa?
Acha aende kuzimu huko hatuitaji msamaha wa mfu

Maisha ndo hayahaya
Na malipo ni hapahapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…