Ushauri kwa Membe, Jitenge na Wanafiki

Ushauri kwa Membe, Jitenge na Wanafiki

Wana JF hapa bongo ivi huyu baba alisharudi kweli?
Kwani kuna siri kwamba alikwapua pesa za michango ya mfuko wa jamii huku wakitunga sheria kuwakwamisha wamiliki halali wa pesa hizo wanapotaka kujitoa baada ya kuchoka na ajira zisizo na tija?
 
Naona unauwekea msamaha mipaka mpaka kuanza kuwaita wale wanaotaka Musiba asamehewe ni wanafiki.

Msamaha ni msamaha tu, bila kujalisha unaombwa muda gani, na wakina nani, lakini sio kuwaita wale wanaokutaka usamehe wanafiki, kwangu huko ni kutafuta kisingizio tu cha kutosamehe.
Ni wanafiki mbona wakati Musiba akiwa anamtumikia shetani Magufuli wote mlikaa kimya hamkukemea?

Wote ni wanafiki pamoja na wewe. Ova
 
Mtu atafute kisingizio cha kutokusamehe kwani mtu huwa analazimishwa kusamehe?

Wanaosema leo kuwa Musiba asamehewe, hakika ni wanafiki:
Musiba alikuwa anatukana watu na kuhamasisha watu wauawe na wengine wavunjwe miguu. Hawa wanaosema Musiba asemehewe, wakati huo walifanya nini? Wemgine mpaka walikuwa wanashangilia, we gine walimsifu, na wengine walikaa kimya. Wote hao hawakuona uovu wowote uliokuwa ukifanywa na Musiba. Msamaha hutolewa kwamtu aliyekosa, sasa hawa ambao walikuwa wakimshangilia Musiba, ni lini yale waliyokuwa wakiyashangilia, wamegundua kuwa ulikuwa ni uovu? Kama walijua toka mwanzo ulikuwa ni uovu, waanze kwanza kuomba msamaha kwaajili yao kwa kuwa wanafiki, kabla hawajamwombea msamaha Musiba.

Katika watu wote waliomwombea msamaha Musiba, ni Askofu Mwamakula pekee ndiye alionekana kuweka bayana kuwa yale yaliyokiwa yakifanywa na Musiba ni miongoni mwa ubatili. Askofu huyu haukutumikia unafiki. Iwe mvua iwe jua; iwe mbele ya mtawala au mbali na mtawala, alisimama katika ukweli.

Shetani humpa mwovu mafanikio ya muda mfupi, hayawezi kuwa ya kudumu. Musiba atakuwa shuhuda mzuri katika hili
Hapa huzungumzii msamaha tena, nakuona unazungumzia kisasi kwa sauti ya juu huku ukikipa jina la msamaha.

Unaonekana upo na mihemko ya kiwango cha juu sana, mpaka unafikia stage ya kumuita mwanadamu mwenzio shetani ukisahau tumeaswa tusihukumu ili nasi tusije kuhukumiwa.

Nawaona wengi wenu hii issue ya Musiba na Membe mnaichukulia kishabiki sana, mmeshindwa kabisa kutofautisha hisia zenu na uhalisia.
 
Naona unauwekea msamaha mipaka mpaka kuanza kuwaita wale wanaotaka Musiba asamehewe ni wanafiki.

Msamaha ni msamaha tu, bila kujalisha unaombwa muda gani, na wakina nani, lakini sio kuwaita wale wanaokutaka usamehe wanafiki, kwangu huko ni kutafuta kisingizio tu cha kutosamehe.
Swali! hao wanaomwombea msamaha Musiba leo wanakerwa na nini? Je wakati Membe na wengine kama vile Kinana, Makamba, Kabwe, Mbowe, Lissu etc, wanasulubiwa na kashfa za uongo na kukera wao walijisikiaje mbona hawakukemea.
 
Kuna kelele nyingi za wanafiki kwako Mh. Membe. Lililo jema ni kwamba unaufahamu sana unafiki wao.

Manabii wa kweli wa Mungu, tangu historia, na tangu kale, wanafahamika kwa kusimama na kuusemea ukweli. Hawakujali nini kitawapata kwa kuwa wakweli. Walismama imara hata dhidi ya wafalme wenye nguvu na wenye mamlaka ya kutisha.

Tuwaulize viongozi wetu wa dini, wakati watu wakishambuliwa kwa risasi, wakiuawa, wakitekwa, wakiporwa mali zao, wakibambikiziwa kesi na kutupwa magerezani kwa uonevu, wao waliokuwa wapi? Walisimama upande upi? Walinena nini juu ya uovu ule?

Mungu aendelee kusimama na viongozi wa dini waliokemea na wanaoendelea kukemea uovu, wanaoutumikia ukweli, kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa ukweli, ni Mungu wa haki.

Ushauri wangu kwako Membe, ili usiendelee kusumbuliwa na watu wanafiki wanaojifanya wana hekima leo, lakini walijifanya vipofu na mabubu wakati uovu unatendeka, toa tamko kuwa iwe ni ofisini kwako, nyumbani kwako au mahali pengine popote, hutaki kutembelewa na mtu yeyote mnafiki ambaye anakuja eti kumwombea msamaha Musiba.

Ikikupendeza ruhusu tu kujadiliana na watu wenye hekima, watu ambao maisha yao yamejawa na kusimama katika ukweli bila ya kujali watawala watanena nini.

Lakini ufahamu kuwa ule uchafuzi wa haiba za watu, uhamasishaji wa watu kuuawa na kufungwa ulikuwa ni mradi uliohusisha watu wengi, mbele wakiwa wamemsimamisha Musiba, wao wakiwa nyuma yake. Hao waliokuwa nyuma yake, wengi wao ndio watakuja sasa na kujifanya washauri wa kukutaka umsamehe Musiba. Na wengine kwa vile hawawezi kukyfikia, wanawatumia viongozi wa dini wanaoamini wanaweza kuwatumia.

Ukweli ni kwamba watu hawa hawaombi umsamehe Musiba kama mtu tu, bali umsamehe mwenzao ambaye walimweka mbele na wao wakiwa nyuma yake. Hawa wanataka kujitoa kwenye mazingira ya kulaumiwa na Musiba ambaye anawaona wamemsaliti kwa kutomsaidia nyakati hizi. Ukimwachia huyu mhalifu, hawa wahalifu wenzake watakwenda na kumwambia kuwa tumefanya kazi, tumekusaidia mpaka umekuwa huru sasa. Mbinu yao kubwa waliyoibuni kwa sasa ni kuwatumia viongozi wa dini ambao wwanawafahamu kuwa kwa namna fulani walikuwa nao katika katika hali ile ya kuulinda uovu.

Waliokuwa na Musiba, wamsaidie Musiba kulipia uovu wake, maana wao ni sehemu yake katika uovu wake. Na baadhi ya watu ambao sio waovu, na hawakuwahi kuwa waovu, wawe na hekima siyo kukubali maombi ya watu hovyo hovyo, hata wakaharibiwa heshima zao kutokana na kutumika na hao waovu wa kundi la Musiba.

Mpaka sasa si Musiba binafsi ndiye anayewaona viongozi wa dini kumwombea msamaha Musiba, bali ni watu wale wenzake na Musiba ndio wanaoenda kwa hao viongozi wa dini.

Mh. Membe, ujaliwe hekima katika hili.

Watu wanafiki Sana wakati Musiba anatukana watu live walikuwa wanachekelea na Wala hawakuenda kumuonya, ila leo amedhibiwa wanamlilia membe amsamehe.
 
Membe kama anataka fidia atalipwa full stop, alaf mambo mengine tusubir mda utupe majibu, wala haina haja ya kunyenyekea, dunia inazunguka hii, hamna haja ya kutishana Sana wakat wote tunakunya
Kweli lazima misiba alipe bilioni 8, tuache unafiki. Member alidharilishwa mkawa mnafurahia, Leo ndio mnajua Dunia inazunguka. Yani uwafanyie wengine ubaya uwachwe kisa Dunia inazunguka?. Alipe pesa za watu huyo chawa.
 
Wewe ulikuwa shuhuda wa mauaji?

Ulimboka, Kibamba, Mwakyembe, Mwandosya, Kubenea, Mwangosi waliumizwa na nani vile? Huyu mbwabwajaji wa Mtama si ndo alikuwa kachero mbobezi na waziri wa anga za juu mbona hukusema yote aliyoyatenda?

Tufe linazunguka sehemu yoyote na wakati wowote.
CCM wote hao majambazi tu. Wauane wenyewe huko.
 
Swali! hao wanaomwombea msamaha Musiba leo wanakerwa na nini? Je wakati Membe na wengine kama vile Kinana, Makamba, Kabwe, Mbowe, Lissu etc, wanasulubiwa na kashfa za uongo na kukera wao walijisikiaje mbona hawakukemea.
Huyo Musiba Kama wote aliowatukana wangemvalia njuga, sijui angesemaje?. Maana amemtukana Sana Lissu na akina Maalim Seif, ila walichukulia poa. Mjinga yule awe fundisho kwa chawa wengine.
 
Manabii wa kweli wa Mungu, tangu historia, na tangu kale, wanafahamika kwa kusimama na kuusemea ukweli. Hawakujali nini kitawapata kwa kuwa wakweli. Walismama imara hata dhidi ya wafalme wenye nguvu na wenye mamlaka ya kutisha.
Kwa kukutajia mifano tu
1. Daudi mbele ya Sauli
2. Eliya mbele ya Ahabu
3. Elisha mbele ya Ahabu
3. Yosia mbele ya Farao
4. Daniel mbele ya Nebukadneza na Dario.
5. Yesu mbele ya Pilato
6. Mussa mbele ya Farao

7.Lissu mbele ya.......😅😅
 
Kuna kelele nyingi za wanafiki kwako Mh. Membe. Lililo jema ni kwamba unaufahamu sana unafiki wao.

Manabii wa kweli wa Mungu, tangu historia, na tangu kale, wanafahamika kwa kusimama na kuusemea ukweli. Hawakujali nini kitawapata kwa kuwa wakweli. Walismama imara hata dhidi ya wafalme wenye nguvu na wenye mamlaka ya kutisha.

Tuwaulize viongozi wetu wa dini, wakati watu wakishambuliwa kwa risasi, wakiuawa, wakitekwa, wakiporwa mali zao, wakibambikiziwa kesi na kutupwa magerezani kwa uonevu, wao waliokuwa wapi? Walisimama upande upi? Walinena nini juu ya uovu ule?

Mungu aendelee kusimama na viongozi wa dini waliokemea na wanaoendelea kukemea uovu, wanaoutumikia ukweli, kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa ukweli, ni Mungu wa haki.

Ushauri wangu kwako Membe, ili usiendelee kusumbuliwa na watu wanafiki wanaojifanya wana hekima leo, lakini walijifanya vipofu na mabubu wakati uovu unatendeka, toa tamko kuwa iwe ni ofisini kwako, nyumbani kwako au mahali pengine popote, hutaki kutembelewa na mtu yeyote mnafiki ambaye anakuja eti kumwombea msamaha Musiba.

Ikikupendeza ruhusu tu kujadiliana na watu wenye hekima, watu ambao maisha yao yamejawa na kusimama katika ukweli bila ya kujali watawala watanena nini.

Lakini ufahamu kuwa ule uchafuzi wa haiba za watu, uhamasishaji wa watu kuuawa na kufungwa ulikuwa ni mradi uliohusisha watu wengi, mbele wakiwa wamemsimamisha Musiba, wao wakiwa nyuma yake. Hao waliokuwa nyuma yake, wengi wao ndio watakuja sasa na kujifanya washauri wa kukutaka umsamehe Musiba. Na wengine kwa vile hawawezi kukyfikia, wanawatumia viongozi wa dini wanaoamini wanaweza kuwatumia.

Ukweli ni kwamba watu hawa hawaombi umsamehe Musiba kama mtu tu, bali umsamehe mwenzao ambaye walimweka mbele na wao wakiwa nyuma yake. Hawa wanataka kujitoa kwenye mazingira ya kulaumiwa na Musiba ambaye anawaona wamemsaliti kwa kutomsaidia nyakati hizi. Ukimwachia huyu mhalifu, hawa wahalifu wenzake watakwenda na kumwambia kuwa tumefanya kazi, tumekusaidia mpaka umekuwa huru sasa. Mbinu yao kubwa waliyoibuni kwa sasa ni kuwatumia viongozi wa dini ambao wwanawafahamu kuwa kwa namna fulani walikuwa nao katika katika hali ile ya kuulinda uovu.

Waliokuwa na Musiba, wamsaidie Musiba kulipia uovu wake, maana wao ni sehemu yake katika uovu wake. Na baadhi ya watu ambao sio waovu, na hawakuwahi kuwa waovu, wawe na hekima siyo kukubali maombi ya watu hovyo hovyo, hata wakaharibiwa heshima zao kutokana na kutumika na hao waovu wa kundi la Musiba.

Mpaka sasa si Musiba binafsi ndiye anayewaona viongozi wa dini kumwombea msamaha Musiba, bali ni watu wale wenzake na Musiba ndio wanaoenda kwa hao viongozi wa dini.

Mh. Membe, ujaliwe hekima katika hili.
Asante sana Bams kwa bandiko hili. Umesema ukweli kabisa. Mtu kama Kardinali Pengo ni mnafiki mkubwa. Leo hii anajifanya ni mtu wa haki wakati enzi watu wanauawa na kuwindwa kwa risasi kama swala alikuwa anakaa kimya! Yule mwovu alikuwa anakaribishwa madhabahuni kila siku na kupewa nafasi kueneza chuki na ujinga wake!
 
Kwa kukutajia mifano tu
1. Daudi mbele ya Sauli
2. Eliya mbele ya Ahabu
3. Elisha mbele ya Ahabu
3. Yosia mbele ya Farao
4. Daniel mbele ya Nebukadneza na Dario.
5. Yesu mbele ya Pilato
6. Mussa mbele ya Farao

7.Lissu mbele ya.......😅😅
Jiwe
 
Back
Top Bottom