Ushauri kwa madiwani wa UKAWA jijini Dar-es-salaam

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,145
144,657
Mkianza kazi, kupitia vikao vyenu vya Baraza la Madiwani kwa kila Manispaa, agizeni maafisa ardhi wawapitie ramani za maeneo yenu na muwaagize wa-identfy maeneo yote ambayo hayakuvunjwa na ambayo yamevamiwa zikiwemo fukwe za bahari n.k na kupitia vikao vyenu vya Baraza la Madiwani, muwaagize Wakurugenzi wa Manispaa kuvunja majengo yote yaliyoko katika maeneo hayo.


Wananchi wa chini wameonya mkono wa sheria na sasa iwe zamu ya vigogo na mali zao pamoja na majengo ya serikali katika Manispaa zenu.

Onyesheni sheria ni msumeno.
 
Hawana sababu ya kuwaagiza maafisa ardhi na kama hujui maafisa ardhi hawapokei maagizo kutoka kwa madiwani....wao wana report kwa kamishna wa ardhi hata kama wapo kwenye halmashauri....halmashauri wapo nazo kwa mambo ya kibajeti tu.

Ila pamoja na hayo...tayari kamishna pia amewataka wale wote ambao wamejenga kinyume na sheria ya matumizi ya ardhi na ile sheria ya mipango miji kuvunja wenyewe majengo yao...na kama hujasoma sheria hizo ...pamoja na mambo mengine...zinazungumzia pia umbali wa kujenga kutoka kwenye fukwe za bahari ambao ni mita 60....sasa wale matajiri wote ambao wamevunja sheria hii basi rungu litawaangukia tu. Hakuna namna.

Kumbuka Dkt Magufuli alitaka kuifyeka TANESCO kwa kuwa tu imejengwa kwenye hifadhi ya barabara....hivyo huyu sio mtu wa kuogopa mtu. Na kama humjui Dkt Kusiluka ambae ndiye kamishna wa ardhi..basi ni vyema ukauliza...huyu mtu hana bei.
 
Hawana sababu ya kuwaagiza maafisa ardhi na kama hujui maafisa ardhi hawapokei maagizo kutoka kwa madiwani....wao wana report kwa kamishna wa ardhi hata kama wapo kwenye halmashauri....halmashauri wapo nazo kwa mambo ya kibajeti tu.

Ila pamoja na hayo...tayari kamishna pia amewataka wale wote ambao wamejenga kinyume na sheria ya mipango miji kuvunja wenyewe majengo yao...na kama hujasoma sheria hiyo ya mwaka 2008...pamoja na mambi mengine...inazungumzia pia umbali wa kujenga kutoka kwenye fukwe za bahari ambao ni mita 60....sasa wale matajiri wote ambao wamevunja sheria hii basi rungu litawaangukia tu.

Kumbuka Dkt Magufuli alitaka kuifyeka TANESCO....sio mtu wa kuogopa mtu. Na kama humjui Dkt Kusiluka ambae ndiye kamishna wa ardhi..basi ni vyema ukauliza...huyu mtu hana bei.
Acha uongo.Madiwani kupitia Mabaraza yao wana Mamlaka hayo.

Tunataka kuona na vigogo wanawajibika na sio porojo zenu.
 
Back
Top Bottom