Ushauri kwa mabinti

Pole mkuu, Sina neno lingine
 
Dude you got issues, go figure them out.
 
Uko sahihi mkuu. Tatizo ni matusi maana mwanaume hata ukimkatalia hawezi kukubaka. Ya nini matusi?
 
Tatizo ni mabinti wachache watakaokuelewa kwa hili mpaka huo umri wa majeruhi utakapowadia. Sasa hivi itakuwa inaingilia sikio moja na kutikea sokio la upande wa pili kama lilivyoingia. Ila ukweli unabaki pale kwamba binti smart hatasubiri yamkute ila atajifunza kwa waliomtangulia.

Naona wengi wanalalamika wakifikiri unajaribu kuwashusha mabinti thamani ila ukweli unabaki ulivyo. Wajanja wanaweza kujifunza kutokana na mawazo ya wanaume kuliko wao kuliwazana humu. Inawezekana wengine umeongea yanayowatesa kwa wakati huu na hawataki kukabiliana na uhalisia. Tumuombe mungu awajalie wepesi maana wengi kwenye kipindi hiki huwa ni kama wanakuwa wameondolewa ufahamu ambao hurudi baada ya muda fulani. Ndiyo maana nasema unaweza usiekeweke sasa hivi ila huo ndo ukweli.
 
Umefafanua vema sana mkuu.........wanasema jambo moja ni heri kusikiliza mafunzo ya mwanadamu mwenzio mara anapokupa tahadhari na ukayafanyia kazi utaepuka maumivu kede huko mbeleni ila usije subiria ufunzwe na ulimwengu maana mafunzo ya ulimwengu hayana maelekezo ila ni mitihani ya mfululizo na hakuna wa kukusaidia kujibu hiyo mitihani lakini pia maumivu ya hiyo mitihani hayana nafuu wala ganzi.

Kiukweli hapa wanaokataa na kupinga ni wale tu ambao wapo bado katika ule umri ambao tunaita hawajapevuka kamili. Katika umri huu ambao mostly ni 17-27 au zaidi wanawake huwa wanafanya mambo ambayo kijamii huwa tunaita ni ujinga. Haya ni matokeo ya kukosekana kwa elimu rasmi juu ya kujitambua kwa rika. Ku rika ukifika hutakiwi kufuatanana wasichana wenzako na unatakiwa uanze kuwa mtu wa kufanya maamuzi binafsi ya kimaisha. Leo hii kuna mdada wa miaka 26 au 27 mwanaume anamfuata kwa nia nzuri tu ya kumuhitaji waishi pamoja ....huyu msichana bila busara wala hekima badala amalizane na huyu kijana kwa kumuomba aende nyumbani kwao akaombe ridhaa kwa wazazi wake na kumposa utashangaa anawapelekea hizi taarifa rafiki zake ambao wataanza kumjadili huyu kijanaas if ni majaji wa mashindano ya mitindo ya nguo. Mwisho wa siku watamshawishi mwenzao kukataa au kukubali kwa vigezo vya kipumbavu kama pesa....uzuri na utanashati wa kimuonekano wa huyu mwanaume na mambo mengine yasiyo ya msingi kama wao kupewa ofa ya kutolewa out na shemeji yao

Kiukweli watoto wa kike huwa mnachukulia simple sana hii kitu ila siku utakapoanza kujitambua kuwa umri unakwenda sidhani kama kuna rafiki ama shosti yako ataweza kukushauri ukatulia akili maana utapanic vilivyo na hautakuwa na ujanja hata kidogo. Hapo ndipo utajua kuwa mbio za sakafuni huishia ukingoni.

Kwasasa utaringia hayo makalio......sura.....ngozi nyororo......sijui nini hivyo vyote huwa vina muda wa kuwepo na vitatoweka taratibu kama vilivyokuja. Sasa wewe kaa tu hapo ukijibu majibu ya kujifariji ukahisi kuwa hii post ni ya majungu......ipo siku utasoma tena hii post lets say miaka kumi ijayo utakuja hapa na kutoa ushuhuda kuwa ni bora ungetilia maanani haya maneno.

Thamani ya mwanamke huenda ikipungua katika muonekano kila anavyoongezeka umri na huongezeka kutokana na tabia nzuri aliyokuwa nayo. Hawa akina shangazi akina mama na mabibi nao walikuwa mabinti kama ninyi ila leo hawana hata uthubutu wa kuringa maana hakuna cha kuringia mvuto wa mionekano yao kwa sasa ni sifuri.

Wanaume wanapokuwa vijana huwa hawanaga mvuto ila umri unavyozidi huwa wanaanza kuwa na umuhimu sana katika maisha ya mwanamke......kwa maana mwanaume ni mwanaume tu. Mimi hapa mwenyewe ni shuhuda......nina binamu dada yangu ambaye alikuwa ni balaa kwa kupanga wanaume. Tena wanajuana. Kuna siku naikumbuka vizuri kabisa alishawahi kuja mwanaume analia nyumbani akimsihi b mkubwa amsaidie kuzungumza na huyu binamu maana amesha mgharamikia sana na amegundua kuwa ana watu wengine nje na alimkana alipomfumania ila jamaa akakubali kuwa mpole na akawa tayari kumpokea tena ila kwa ngebe huyu dada binamu alikataa hilo ombi jamaa aliondoka anatia huruma hadi leo nikikumbuka ile picha ninaumia sana maana yule ni mwanaume kama mimi na alikuwa na haki kwakweli sema nilikuwa mdogo ila ningemshauli yule dada binamu amkubalie maana jamaa alikuwa mtu poa sana. Ila yule binamu akacheza na maisha ya ujana akaja kujihusisha na mume wa mtu alipoona umri unakwenda. Jamaa akampa ujauzito akampangishia nyumba nzima. Mkewe akaja kujua akamuendea ustawi wa jamii jamaa akawekwa kitako akapewa masharti kuwa atasimamishwa kazi halafu pesa na mali zote zitakabishiwa kwa mkewe na watoto. Kisha akirejea kazini nusu ya mshahara atapewa mke na watoto yeye akafute maisha.mapya. Jamaa akaona isiwe kesi akatubu akairejea familia yake.......hadi leo nawapa huu mchapo ameokoka na analea mtoto pekee yake jamaa hana time. Hana mume anaishia kukaa na vijamaa visivyo na mbele wala nyuma vinamfariji na sidhani kamakuna dalili ya kuletewa shemaji wa maana tena na sasa ana umri wa 33.

Sasa usije ona watu wanazungumza hivi vitu ukadhani wanatunga.......vinawatokea akina dada wenzako wewe kaa ukihisi ni malaika ila ipo siku haya maneno yatakuwa na maana kubwa kama yule mwanafunzi aliyekuwa akiambiwa na mwalimu wake wa hisabati kuwa ajibidiishe katika kufanya mazoezi ya hisabati ili afaulu mtihani wa kidato cha nne na akachagua kuzembea na kuchukulia poa kisha akaja kushituka usiku wa jumapili ambao jumatatu mtihani wa kwanza ni hisabati na hakuna kinachokwenda hapo akisoma past pepers za NECTA . Tena bora huyu atarisiti atapofeli......wewe ukifeli hakuna kurisiti katika maisha ya binadamu ukiyachuma majanga utayabeba na familia yako. Sasa wewe kaa na hizo jeuri na kauli za kujifariji unazochukua kwa rafiki zako ambao hamtakuwa wote siku maji yakiwa ya shingoni.

Kalaga baho......message sent and delivered.
 
Mwanaume hatukanwi.mwambie tu sawa nimekusikia na ninakupenda pia. Then tazama hatua inayofuata,utajua anahitaji nini kwako. Baada ya hapo ni akili mkichwa.
 
Huo ushauri peleka kwa Dada zako, humu kila mtu anaishi anavyotaka na wote tuna akili timamu za kufanya maamuzi. Usitupangie namna ya kuishi.
Mshaona ili kupata kiki ya kutokea humu lazima muanzishe maujinga ya khs wanawake.
Mtuache tufanye yanayofurahisha mioyo yetu.
 
Bila shaka hujuelewa vema mada. Hapo mtoa mada ameeleza kinaga naga kuwa si lazima mwanamke amtukane mwanaume aliyemtongoza ima amkubalie.
Anaweza kumkatalia ila kwa lugha laini tu. Naunga mkono njia hiyo kwani hata kama mtonhozaji alikuwa na mpango nawe hatokwazika na kukuombea mabaya
 
Ana lugha tamu mpaka raha... Anajua sana kudeka... Nampenda sana...


CC: Kasinde

Nakupenda sana mpenz wangu wa moyo...
Hakika wajua kunidekeza na kunibembeleza....
Kwako nimefika mapenzi yangu kwako ni mapya kila uchao....

........ I love you more and more.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…