kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,872
Kwanza nawasalimu wote,
Kama mada inavyojieleza napenda kutoa ushauri huu kwa dada zetu.
Ukiwa msichana kutongozwa ni jambo la heri ila si lazima kila anayekutongoza umkubalie, bali inatakiwa mwenyewe uchunguze kwa makini zile sifa stahiki unazozitaka kwa mwanaume iwe kwenye mapenzi au kwenye ndoa ili ufanye maamuzi sahihi.
Kumekuwa na wadada wengi sana kulilia kuolewa kwasasa mpaka wanaenda makanisani kuombewa ili wapate wanaume. Lakini si kweli kwamba hawa mabinti toka awali hasa kwenye umri wao wa miaka 19-26 hawakutongozwa na watu walio serious kabisa.
Wengi wao walitokewa na watu, wengine walifanya watu wasafiri kutoka upande moja wa nchi hadi mwingine ili tu waonane, wengine waligharimu wanaume kwa namna tofauti kuanzia pesa hadi muda ila mwisho wa siku wakawabwaga hao wanaume, au kurubuniwa na wengine.
Kuna wasichana ambao kila walipotongozwa walitukana hao waliokuwa wanawatongoza, waliwaporomoshea matusi vijana wa watu na kuwavunja moyo. Kiukweli mwanamke hapaswi kumtukana mwanaume pale anapotokewa bali kumjibu kwa lugha nzuri hata kama huyu jamaa ni king'anga'anizi. Nina mifano mingi sana ya wasichana ninaowafahamu ambao leo hii wanalilia kuolewa ila walipokuwa kwenye peak walikuwa wanatukana wanaume kila aina ya tusi pindi wanapotongozwa.
Unakuta mwanaume anajitolea muda wake, vocha na gharama zingine kwa ajili yako tena seriously halafu unamtukana halafu unashinda kanisani Mungu akupe mume bora kwani huyo anayekusumbua si bora?, Na kama unamuona si bora kwanini usimuombee kwa Mungu ili awe bora kwako.
Mwisho napenda kuwaasa akina dada kuacha kabisa kuwatusi wanaume pale wanapotongozwa na kukosoa wanaume utafikiri nyie mnaweza kumuumba mtu halafu baadaye umri unapokwenda mnaanza kulialia na kumuuliza Mungu why mimi.