Ushauri kwa mabachela wenzangu kuhusu "Single Mother"

Ushauri kwa mabachela wenzangu kuhusu "Single Mother"

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,309
Reaction score
15,294
Oya wana, mkiwa tayari kuingia kwenye Mapenzi au (Ndoa) Hakikisha unaepuka kiaina Masingo Maza.

Acheni Masingo maza waolewe na masingo faza wenzao.

Kuna sababu kadhaa ambazo nimekuja kugundua kuwa sio poa kabisa kwa afya zetu sisi Mabachela.

1. Itakuhitaji uanze kujifunza kuwa baba mapema zaidi kuliko kawaida.

2. Mfupa alioushindwa Fisi wewe unauwezaje?

3. Hata kama fisi kaushindwa huo mfupa, kuna BOND fulani hivi iliyopo na itaendelea kuwepo katiya Singo maza na huyo Fisi. Hivyo basi Fisi huwa atakuwa na tabia ya kurudi rudi kwa lengo la kuutembelea mfupa uliomshinda (Mshaelewa kitu hapa).

4. Hivyo basi masuala mengi yatakayokuwa yakizungumzwa baina ya fisi na Singo Maza yatakuwa yanawahusu wao na mtoto wao sanasana. Wewe utakuwa wala sio kipaumbele kwenye mahusiano.

5. Sindo Maza anakuchukulia kama tairi ya ziada (spare wheel). Muda wowote ule Fisi akishinda BIKO wewe unaachwa solemba. LOL

6. Siku moja unaweza kuambiwa kuwa "Unapiga huyo mtoto ni wako?"

7. All in All Ni kama kununua shamba ambalo liko na kesi Mahakamani ambapo huna uhakika wa umiliki nalo.

single-mother-e1563464853694-760x427.jpg
 
Umemaliza?
Na vipi kuhusu Single Dad kuoa mke asiye na mtoto?
Wakati Mwingine wanaume tuache ubinafsi
Ushaambiwa single mother ni kama shamba lenye kesi mahamakani,usilinunue,sasa huo ubinafsi unatoka wapi au bado hujaelewa maana ya shamba ?
 
Tatizo la masingo maza ni tamaa tu inayowasumbua. Mwanamke yuko radhi azae na muuza unga, jambazi, kinaka, mchawi, kwa tamaa na sifa za kijinga kwa mashosti wake kuwa kapata mtu mwenye hela. Akija achwa ama jambazi lake kuuliwa na kukosa hela anaanza kuhaha kutafuta mwanamme wa kumasakizia mtoto amlee na kumpa majukumu ya ubaba wakati mtoto si wake. Sitaki kabisa kudili na mwanamke mwenye watoto aliyezaa na vibaka ama wauza unga nije kulea mie.
 
😀😃😀😃 Subiri wenyewe waje
 
Acha kuwatisha watu. Kurudiana kati ya watu walio achana kunategemeana na akili zao. Siyo wote huwarudia wapenzi wao wa zamani. Ni dhambi kubwa kujenga hofu kwa wapendanao, kisa tu umeumizwa baada ya kuparamia sehemu ambayo haikuwa sahihi kwako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom