Ushauri kwa Lowassa

Ushauri kwa Lowassa

Unaota...meli karibia inatia nanga..hapa ni mabadiliko tu hakuna namna nyingine
 
Lowasa nakushauri sana uachane mapema na mbio zako za kuutaka uraisi. Sababu kundi kubwa la viongozi wa CCM halikutaki, waliokushauri wamekudanganya.

Jina lako litakatwa mapema kabla ya fainali!! Ukiangalia mpaka sasa hivi umeshatumia hela nyingi sana na mda mwingi sana kwa ajili ya kujisafisha na kujijenga kwa ajili ya kuwania urais.

Kabla mambo yasijekuwa mabaya zaidi, ningekushauri haraka sana ondoa jina lak ktk kugombea uraisi na ukajiunge rasmi chama cha ACT-Wazalendo ambako mda mrefu umealikwa.

Kwa kufanya hivyo utakuwa umetoka na kundi kubwa la wana CCM na kuhamia huko..Na hata kama hutafanikiwa kupata uraisi safari hii lakini safari ijayo huenda ukafanikiwa.

Endapo utang`ang`ania CCM na jina lako lika katwa basi ndoto yako ya kuwa rais itakuwa imezimwa maishani na hata kama utaamia upinzani baada ya kutemwa hautang`ara tena, utakuwa kama akina Mrema!

Usiwafuate hao wapambe njaa akina Kingunge na wengine.

Hao wako kimaslahi zaidi wanataka kula hela zako tuu

Hata wewe CCM haikutaki ndio maana mpaka leo Haujapata maisha bora.
 
Nakuhakikishia, hata kila m-ccm angelichukua fomu, LOWASA ni kisiki cha mpingo. Mtajikwaa na kung'oka meno hatoki wala hakatwi. Huyo ndo rais wa ccm. Lowasa ndo ccm na ccm ndo Lowasa. Anayemchukia aondoke ccm amwachie mwenyewe. Hiyo ndo habari ya leo. Hao wanachukua fomu ili wampishe mwenye hicho kiti. Ni wapambe wa biarusi hao, wakiwa wengi harusi hunoga zaidi. Mark ma word

aiseeeeee
 
Back
Top Bottom