Ushauri kwa Kampuni itakayoshinda zabuni ya kutoa huduma ya Mwendokasi

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,067
2,222
Kampuni hiyo isithubutu kuajiri au kuwarithi wafanyakazi waliokuwa kwenye Kampuni ya UDART. Njooni na Wafanyakazi wenu wapya, kwenye interview mkimhoji mtahiniwa na akasema yeye alikuwa UDART, asipewe kazi kabisa

Kwa sababu wafanyakazi wa Kampuni hiyo ni wa hovyo, wasikojua customer care wala kujali Mali za ofisi. Wana lugha mbaya wasiojua Time table, hawana ubunifu na Mwisho ni wabadhirifu.

Kuanzia Mameneja, Madereva hadi wasimamizi wa vituo wote hawafai.

Kampuni mpya itakayoshinda zabuni hiyo tafadhali zingatieni hayo na pia msikubali kuajili wafanyakazi kwa Vi memo vyovyote, mtaharibu biashara yenu.
 
Wazo lako ni zuri lakini Lita athiri pakubwa. Binadamu ni wale wale ata ikitokea wamebadilishwa. Cha msingi ni sera na sheria yani in short mwongozo.

Waje na mwongozo mpya, the whole operating system has to change which means haito hitaji na watu wabadilishwe.

Kila taasisi imara Ina Operating system people come and go lakini OS inabakia.

Kwa kusema hivyo, Mwekezaji mpya aje na Strong Operating System itakayo cover madudu yote ya UDART kwasab yeye alikua nje anaona na data zinadhihirisha ilo. Asante
 
Kwa hiyo mkuu hutaki watanzania wenzako wapate ajira ?

Au kunasehemu utawapeleka wakafanye kazi na wajipatie ujira na mshahara ?

Shida sio wafanyakazi bali ni mifumo

Jiulize kwa nini kipindi cha JPM watumishi wa umma kama sio wote walikuwa angalau wanatimiza wajibu wao , na alipofarika ghafla hali ikabadilika huku watu ni walewale na nafasi wanazohudumu ni zilezile ?
 
Kampuni ya maana itachukuwa haojao na wengi wao watabadilika na kuwa na mitazamo mipya.

Asiyekidhi vigezo na kufata mfumo mpya ndiye wa kuondolewa.
 
Mkuu hapo tatizo ni management tu ,waweke mamanagers/supervisors wa kwao.

SUpervisor wa kila kituo(Mwisho) ahakikishe hakuna abiria wanaosubiri kwa muda mrefu kwenye vituo ,gari ikija supervisor ndiyo anadecide dereva achukua route ipi kulingana na mahitaji....Maana kwasasa hao madereva wakifika wanapaki tu wanakaa huku abiria wanajazana vituoni.
 
Usimamizi na uwajibikaji ukiwa mbovu katika mradi wowote ule ;uwe ni serikali au shirika binafsi.. mambo huenda mrama.
 
Watu wa Dubai walishapewa kazi na nauli watapanga wao. Usitegemee Latra watamtetea mlipa Kodi wa Tanzania.
 
Kwa hiyo mkuu hutaki watanzania wenzako wapate ajira ?

Au kunasehemu utawapeleka wakafanye kazi na wajipatie ujira na mshahara ?

Shida sio wafanyakazi bali ni mifumo

Jiulize kwa nini kipindi cha JPM watumishi wa umma kama sio wote walikuwa angalau wanatimiza wajibu wao , na alipofarika ghafla hali ikabadilika huku watu ni walewale na nafasi wanazohudumu ni zilezile ?
Ndiyo maana nikasema hao wenye asili ya UDART,wasiajiliwe,wapo Watanzania wengine ambao hawana ajira,wao ukiwapa mfumo uendeje watatimiza,Siyo hao ambao tayari wameshakuwa na vimelea vya kuharibu badala ya kujenga.Ukiwaajili hao, akili yao ipo tuned kwenye ubadhirifu na uzembe kwa sababu ndivyo walivyozoea.
 
Mkuu hapo tatizo ni management tu ,waweke mamanagers/supervisors wa kwao.

SUpervisor wa kila kituo(Mwisho) ahakikishe hakuna abiria wanaosubiri kwa muda mrefu kwenye vituo ,gari ikija supervisor ndiyo anadecide dereva achukua route ipi kulingana na mahitaji....Maana kwasasa hao madereva wakifika wanapaki tu wanakaa huku abiria wanajazana vituoni.
Nakuunga mkono kabisa.Watanzania waajiriwe kufuta vioo,kuosha Magari na kusafisha Maliwatoni tu.Basi!
 
Back
Top Bottom