Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Mh.Raisi na kamati yako,mnaweza kuhukumu watanzania hawa wanaohoji taarifa ya kamati kuwa si wazalendo,wamejaa chuki na wivu wa kisiasa tu.
Mh.Raisi,ka naomba msifike huko bali eleweni jambo moja tu kuwa watanzania hawa walianza kuumia tangu tangu siku nyingi kuhusiana na hii mikataba na hata utekelezaji wake unavyofanyika ambao unaonekana kuongeza maumivu zaidi.
Mh.Raisi,tambue ripoti ile sasa ni kama imetibua nyongo na kutia watu hasira na machungu hasa wale waliokuwa wakidharauliwa na kubezwa wakati walipokuwa wakipaza sauti kupinga mikataba hii na kutaka ipitiwe upya.
Mh.Raisi,kingine kinachokera na kuudhi ni watu wa chama chako kuanza kujitokeza hadharani ssa na kuanza kubeza wapinzani ambao ndio wemekuwa mstari wa mbele kupinga hii mikataba.Matokeo ya kejeli zao ndio reaction hii unayoiona mitandaoni na kwingineko.
Mh.Raisi,ushauri wangu kwako piga marufuku watu wa chama chako kugeuza swala hili kuwa ni swala la kisiasa vinginevyo usitarajie support ya aina yoyote kutoka kwa wapinzani ambao sasa wameanza kuitwa wapuuzi na ukirihusu hali hii basi uwe tayari kwa yatakonayo.
Ushauri mwingine.Mh.Raisi,kamati yako bado ina nafasi ya kutoa clarification kwa umma in case inaona haikuleweka na wengi vinginevyo ikiri hadharani mapungufu yanayohojiwa katika taarifa hiyo na ikibidi iombe radhi kwa usumbufu waliosababisha.
Mh.Raisi,naomba leo nitoe siri moja kuwa japo mimi ni miongoni wa watu ambao huwa nakupinga sana, ila ukweli ni kuwa kuna saa huwa nakuhurumia sana ila kisichonifurahishi ni wewe kushindwa kuweke taratibu,sheria na mifumo ambayo itasaidia kudhibiti mambo haya kama vile Kutupatia katiba ya mzee wa Warioba,mikataba kupelekwa Bungeni, n.k na matokeo yake huwa nashindwa kabisa kuelewa ni nini hasa dhamira yako katika kusaidi hii nchi kama kweli una nia hiyo japo ni kweli kuna nyakati huwa nakuhurumia sana kama nilivyoeleza hapo juu.
Mh.Raisi,kutoonyesha nia ya kuweka mifumo ya kudhibiti wizi na ufisadi na badala yake kutaka kila kitu kifanyike kwa maagizo yako kunatupa hisia za kufanya mambo kisiasa zaidi na hivyo kukufanya upoteze credibility.
Mh.Rais, kwa uchungu naomnba nimalizie kwa kusema.
Baada ya ripoti ya kamati kutoka,watu wenye akili kubwa hivi sasa wako msibani na wale wenye akili ndogo wako harusini.