Ushauri kwa hili mwana MMU

Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,643
3,875
Habari zenu wana jf....
Mim ni binti mwenye umri chini ya miaka 25 nina mpenzi ambae amenizidi kiumri na pia tupo mikoa tofauti tofauti na wote ni waajiriwa tatizo lililo nileta hapa ni mpenzi wangu huyu ananing'ang'aniza tuzae na mimi sipo tayari kuzaa kabla ya ndoa nimemshauri kama anataka tuzae afuate taratibu zote tukishawekana ndani ntamzalia. Sasa yeye hanielewi au niachane nae tu atafute alie na utayari wa kuzaa? Maana kwa sasa nipo njia panda

NB;KUMPENDA NAMPENDA NAAMIN NAYEYE PIA ANANIPENDA SANA TU
 
USIKUBALIIIIIII! KWANINI ASINGANGANIE AKUOE AMESHAKUONA HADHI YAKO BABY MAMA. Endekeza mapenzi ujinyosoe na upupu. Mwanaume akikuzalisha anakuringia hatariii. Yaani usifanye huo upuuzi.
 
mtu kama hataki kuja kujitambulisha ni NYOKA mwenye sumu kali akikung'ata lazima akuachie alama ya maishan, alaf hiyo long distance love huwa mbaya mchana au ata usiku mtakesha kwenye simu mkichat wenzio wanakesha wakisex mbaya sana huaga siiamin utasikia baby nipo bize hahahah kumbe bize yakukamuana lol,.
 
Hauko tiari kuzaa kabla ya ndoa!!!? Uwe tiari kuletewa mtoto wa nje...

Kwa maisha ya siku hizi vijana kuingia kwenye ndoa itachukua muda ila sio kupata mtoto....
 
Hiyo njia panda labda ya clouds fm lakini yako mwenyewe hapo juu umesema atafute wa kuzaa nae sasa hiyo njia panda ipi?
 
Sawa dada angu asante kwa ushauri
USIKUBALIIIIIII! KWANINI ASINGANGANIE AKUOE AMESHAKUONA HADHI YAKO BABY MAMA. Endekeza mapenzi ujinyosoe na upupu. Mwanaume akikuzalisha anakuringia hatariii. Yaani usifanye huo upuuzi.
 
Hahaha mmh mbona unanitisha jamani
mtu kama hataki kuja kujitambulisha ni NYOKA mwenye sumu kali akikung'ata lazima akuachie alama ya maishan, alaf hiyo long distance love huwa mbaya mchana au ata usiku mtakesha kwenye simu mkichat wenzio wanakesha wakisex mbaya sana huaga siiamin utasikia baby nipo bize hahahah kumbe bize yakukamuana lol,.
 
Baki na msimamo wako uje upate wa kukupa heshima unayostahili kubali maumivu ya muda kataa maumivu ya milele
 
Wewe binti "USITHUBUTU", Narudia tena " USITHUBUTU , kuzaa kabla ya ndoa. Hawa kwa kufanya watoto wa wenzao incubators hawajambo, subiri sasa ubaki single mother ndo utawajua vizuri. Kama ana uwezo wa kukutunza wewe na mtoto, basi ana uwezo wa kuitunza familia yake. Aende kwenu, mfuate taratibu zote muoane. Kuwa na msimamo mdogo angu, atajifanya kulalamika sijui kujinunisha, muache hivyo hivyo. Usidanganyike ooh sijui ananipenda mmmh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom