Ni yamkini kabisa chama cha mapindizi kina rudi nyuma tena kwa kasi ya ajabu, wanachama, makada wanakikimbia chama kwa maelfu, maeneo ambayo yalikuwa salama kwa chama cha mapinduzi usalama umepungua sehemu ingine usalama unaisha kabisa , kwa mfano meeneo kama Pwani, Marogoro, Dodoma, Singida na Tabora yalikuwa salama kwa CCM lakini kama Morogoro usalama umeisha kabisa.
Viashiria (indicator)
Kina viashiria vingi tu vinavyoonyesha CCM inaenda alijojo siwezi kuvitaja vyote labda makada wenzangu muongezee viashiria vingine.
Ni nini sababu?
Hapa ndipo patamu, kwanza nauliza swali hivi kampuni ikifirisika aulizwe nani walinzi wa geitini au utawala? Utawala wa sasa wa chama cha mapinduzi amapo tunashuhudia wanachama na makada wanatimka kwa maelfu kwani ukoje? Kwani umeishiwa mbinu?
Matatizo ya kiufundi (technical problem) yanayokikabili chama cha mapinduzi.
Kutokana na baadhi ya sababu nilizozitaja hapo juu nina shauri Chama cha mapinduzi kichukue hatua zifuatazo bila kuchelewa.
Chama kifanye hayo matatu sasa otherwise they will find it too late. Kikiacha mambo yaendelee hivi hivi chama kitaendelea kushinda lakini kwa nguvu kubwa za polisi siyo kwa ridhaa ya wanainchi, watawachosha sana Polisi. Ikumbukwe Idd Amin alishaanza kuonyesha dalili ya kumpindua Rais Milton Obote siku 60 nyuma Obote akawa anahunyahunya tu kuchukua hatua ni nini kilitokea?
Ninasisitiza chama cha mapinduzi chukueni hatua hizo mala moja bila kuchelewa mda siyo rafiki yenu kabisa.
Viashiria (indicator)
- Mkoani Tabora makada wa CCM wamezomewa mchana kweupe
- Mkoani Morogoro (Ifakara) kadi za CCM zimekokwa moto na moto umewaka kuliko kuni kwa maana zilikuwa kadi nyingi.
- Katika chaguzi ndogo za madiwani CCM inapokonywa kata na wapinzani mfano uchaguzi uliopita tunasubiri tu uchaguzi wa kata nne za mkoa wa Arusha kama CCM haitachukua kata hata moja basi ni wazi kabisa uchaguzi huo CCM imeshindwa na wapinzani.
- Mkoani Manyara makada wa CCM wamefumaniwa wanatoa rushwa guest.
- Dodoma CCM inabebwa sana na daftari la wapiga kura, daftari likiboreshwa Dodoma CCM itazungumza mambo mengine.
- Mkowani Pwani CCM inaanza kwenda kwa wachawi kutafuta uchawi.
- Bungeni wanainchi wanaitana kama tu mpinzani anazungumza, mfano mume kama yupo sebuleni anikimwona Tundu Lissu anachangia hoja anamwita mkewe jikoni mama Fulani njoo umwone Tundu Lissu anazungumza wakati wachangiaji wa CCM hata TV zinafungwa maana wanajamii wanawaona kama uchuro tu
Kina viashiria vingi tu vinavyoonyesha CCM inaenda alijojo siwezi kuvitaja vyote labda makada wenzangu muongezee viashiria vingine.
Ni nini sababu?
Hapa ndipo patamu, kwanza nauliza swali hivi kampuni ikifirisika aulizwe nani walinzi wa geitini au utawala? Utawala wa sasa wa chama cha mapinduzi amapo tunashuhudia wanachama na makada wanatimka kwa maelfu kwani ukoje? Kwani umeishiwa mbinu?
Matatizo ya kiufundi (technical problem) yanayokikabili chama cha mapinduzi.
- Kitengo cha uhamasishaji kama kile kilichokuwa kinaongozwa na kapteni John Komba kimekufa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa.
- Kuiga mbinu, chama cha mapinduzi kimekuwa kikiiga mno mbinu za wapinzani chama kinashindwa kubuni mbinu zake chenyewe.
- Nguvu kazi vinara au front line personnel hawana mvuto, wahuni, hawana mbinu mbinu zao za kizamani wanategemea mno kizazi kinachokwisha, hawachangamkii kizazi kipya, wenzao wamewahi kizazi kipya.
- Matajiri wamekizonga mno chama cha mapinduzi wamekikaba sana shingo chama hakipumuwi wala hakihemi matajiri wamekikalia kooni sasa masikini au mafukara wanakiangalia tu chama cha mapinduzi wanashindwa kusaidia.
Kutokana na baadhi ya sababu nilizozitaja hapo juu nina shauri Chama cha mapinduzi kichukue hatua zifuatazo bila kuchelewa.
- Kumfukuza kazi na uanachama wa chama hicho kada wake Nape Nnawie..
- Kumwondoa mala moja katibu mkuu Col Abdulahiman Kinana
- Naibu katibu mkuu Tanzania bara Mhe. Mwigulu Nchemba apewe karipio kali na wadhamini wa chama huyo hada anaweza kurekebishika lakini Nape Nnawie his damage is beyond repair afukuzwe tu