nimepitia tovuti ya chadema sasa hivi haraka haraka na kushindwa kupata idadi ya wanachama wao. Sasa nawaomba mfanye kama msemo huu unavyosema "mtoto wako mkabidhi kwa mchawi"/ "zimwi likujuwalo halikuli likakumaliza". Vituo viko vya kupigia kura viko karibu 52,000. Hivyo mawakala 52,000 wawe wanachama wa chadema. Pia kuwe na mawakala mbadala 52,000 standby nao vile vile wawe wanachama. Msijindanganye kuwa ambako hamjasimamisha mgombea ubunge kusiwe na mawakala wenu, kumbukeni kura za urais, dr. Slaa.
Mawakala wawepo muda wote wakati wa kufungua kituo, kupiga kura, kuhesabu kura, kubandika matokeo na kupata nakala ya matokeo na kuiwasilisha kwenye chama; mawasiliano ya simu yawe muhimu sana hasa kwenye kujua matokeo ya kila kituo [wakala ampatie matokeo ya kituo kiongozi wa kata au jimbo wa chama kama yupo kama hayupo basi awekwe mtu wa kufanya kazi hiyo ambaye atajumlisha matokeo yote ya jimbo katika ngazi ya urais, ubunge na kata]; chakula kiwe cha safari na kitoke sehemu maalum yenye usalama; mawakala watakao choka au kupata dharura watoe taarifa mapema hili wale mbadala wachukue nafasi; wawe na maji ya kunywa ya kutosha; wasikubaliane na kutokuwepo kituoni au shughuli ya kura kusimama kwa kisingizio cha break ya kwenda kula (hasa baada ya kituo kufungwa yaani wapiga kura kumaliza kupiga kura).
Kwa kweli nimeimba sana kuhusu ili, na nafikiri chadema wameliona na kusoma na kuelewa.